Kocha Jose
Mourinho wa Chelsea wiki hii ameonekana sana kutetea uamuzi wake wa kumsajili
mshambuliaji na nahodha wa Colombia, Radamel Falcao Garcia.
Akionekana
kujipa moyo kutokana na kutofanya vizuri kwa mshambuliaji huyo msimu uliopita
akiwa Old Trafford, Mourinho anadai Falcao hana tatizo tena la majeruhi.
Mourinho
alienda mbali na kusema, kama Falcao angekuwa bado hajapona, wasingepoteza pesa
kumsajili ingawa ni kwa mkopo.
Hata hivyo
kocha huyo ametoboa siri ya kilichosababisha usajili wa mshambuliaji huyo
ukamilike.
Mourinho anasema aliomba ushauri kutoka kwa walinzi wake John Terry
pamoja na Gary Cahil.
Jose anasema
kuwa, Cahil na Terry walimshauri kwamba hata walipokutana na mchezaji huyo, bado
alikuwa na 'movements' za hatari na kwamba anaweza kufunga magoli mengi akipewa
nafasi.
Mourinho
amekaririwa mara kadhaa akisema, anasikitika kuona kuwa watu wanafikiri kwamba
Falcao yule wa Manchester United ndiye halisi. Jose anasema katika makali yake
Falcao hana mfano wake.
Wote
tunasubiri kuona kamali hii ya Mourinho kama itazaa matunda msimu huu.
0 comments:
Post a Comment