Gwiji wa
zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Zinadine Zidane ‘Zizou’
amepongeza uteuzi wa kocha wa zamani wa Liverpool Rafael Benitez kukinoa kikosi
hicho, lakini amemuonya kuwa lazima ashinde
ubingwa wa ligi kuu ‘La Liga’ msimu huu
ili awe na maisha mazuri Bernabeu.
Real Madrid
hawajashinda kombe hilo la ligi tangu mwaka 2012 walipotwaa wakiwa na kocha wa
sasa wa Chelsea, Jose Mourinho.
Rafael
Benitez amesaini mkataba wa misimu mitatu kuifundisha timu hiyo akipokea mikoba
ya Carlo Ancelloti aliyefukuzwa msimu huu baada ya kushindwa kushinda angalau
kikombe kimoja.
Zidane
anaamini Benitez anajua kinachotarajiwa kutoka kwake kwenye timu hiyo aliyaonza
maisha yake ya ukocha miaka ishirini iliyopita.
“klabu
imemsajili Benitez, ni maamuzi mazuri. Lazima kuheshimu uamuzi huo. Benitez ni
mwalimu mzuri lakini matokeo ndio kila kitu” Zizou ameliambia gazeti la Marca.
“Anayajua
mazingira ya hapa vizuri. Anajua kilichopo mbele yake. Kushinda tu makombe ndio
kila kitu hapa.”
Benitez
amewahi kutwaa ubingwa huo wa La liga mara mbili akiwa kocha wa Valencia miaka
kadhaa iliyopita.
Jina la
Zidane lilikua miongoni mwa waliotajwa kurithi mikoba ya kocha Muitaliano Carlo
Ancelloti lakini Zizou amesema anahitaji kuendelea kukinoa kikosi cha Madrid
Castila ili kupata ujuzi na uzoefu zaidi.
“Imekua ni elimu nzuri. Ni changamoto tofauti na kufundisha kikosi cha kwanza.
Tunahitaji kupanda daraja sasa na Real Madrid Castila” anaeleza Zizou “Nimeamua
kubaki hapa kwani Madrid ni sehemu nzuri sana nahitaji kuchangia kitu muhimu
hapa” amemaliza Kiungo huyo wa zamani wa timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment