Friday, June 12, 2015

Hizi ndizo tuzo zilizokuwa zinagombewa kabla hazijaanza kukabidhiwa kwa wahusika jana

BAADA ya minong’ono kuzuka juu ya watu waliopewa tuzo jana hususani kocha bora na golikipa bora, Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi (TPLB), Boniface Wambura amefafanua namna walivyopata washindi.
Mbwana Makata (Prisons) ameibuka kocha bora wa VPL baada ya kuwashinda Hans van der Pluijm (Yanga) na Goran Kopunovic (Simba).
Shaban Hassan Kado naye ameibuka kipa bora akiwabwaga Said Mohamed (Mtibwa Sugar) na Mohamed Yusuph (Prisons).
Wambura amesema mchakato wa kuwapata washinda ulianza wakati ligi inaanza na katika kila uwanja unaochezewa mechi za ligi kuu kuna wataalamu wanaochunguza mwenendo wa wahusika.

“TFF na bodi ya ligi tuna watu wa ufundi ambao wapo viwanja vyote ambavyo mechi za ligi kuu ya Vodacom huchezwa. Kuna vigezo ambavyo wataalamu hawa wanavyo katika kuchagua wachezaji, makocha, timu, golikipa bora na mwamuzi bora. Vyote vinaangaliwa kwa kuzingatia vigezo ambavyo vipo”. Amesema Wambura na kuongeza: “Lakini katika vigezo vyote, kuna kigezo ambacho kipo katika vipengele vyote ambacho ni nidhamu ndani na nje ya uwanja, huu ni mchezo wa kiungwana ‘Fair Play’ , lazima tufike mahala tutambue kuwa nidhamu ndio kitu muhimu katika kufanikisha mpira wa miguu na michezo mingine kwa ujumla”. 

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video