Mbonde (kulia)
Matarajio ya beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salum Mbonde
kutua Yanga yameyeyuka ghafla.
Simba ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kumuwania beki huyo
tegemeo wa Mtibwa Sugar kabla ya Yanga kutupa ndoano zake.
Yanga ilitaka kumsajili beki huyo kwa ajili
ya kuimarisha safu ya ulinzi ya kati kabla ya kumnasa beki wa KMKM ya Zanzibar,
Hajji Mwinyi kwa dau la shilingi milioni 15.
Salehjembe ameripoti kwamba, chanzo cha habari kutoka ndani
ya benchi la ufundi la timu hiyo, kimeeleza beki huyo ameondolewa kwenye orodha
ya wachezaji watakaosajiliwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Chanzo hicho kilisema beki huyo alianza mwenyewe kujiondoa
kwenye usajili wa Yanga kutokana na kuleta mapozi wakati akihitajika.
“Hivi sasa anaomba mwenyewe kusaini kuichezea Yanga wakati
tayari jina lake limeondolewa kwenye usajili wa msimu ujao.
“Awali, wakati tukimhitaji alikuwa akileta pozi kwa
kutopokea simu na wakati mwingine alikuwa akizima kabisa kwa makusudi, hivyo
tumemuona ni kama mchezaji msumbufu, hata kama akija atatusumbua tu.
“Hivi sasa anatusumbua kwa kutupigia simu akiomba asajiliwe
kwa dau dogo la Sh milioni 20, tofauti na awali alipotaka kusajiliwa kwa
milioni 30,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha,
kuzungumzia usajili wao alisema: “Sisi bado tunaendelea na usajili kwa wale
wachezaji tunaowataka pekee, ukiona mchezaji tumemtambulisha, basi ujue
tumemsajili, ukiona kimya ujue hatusajili.”
0 comments:
Post a Comment