Baada ya kutangazwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Al Sadd ya Qatar, Xavi ameongea na vyombo vya habari vya Hispania leo hii na kuelezea kitu ambacho kilijitokeza kwenye basi la Barcelona wakati wanashangilia ushindi wa UEFA Champions League.
Kwenye video iliyosambaa kwenye mitandao anaonekana Xavi akimsukuma usoni Neymar wakiwa kwenye hilo bus. Video hiyo imetafsiriwa kwamba kulitokea ugomvi kati ya wachezaji wakiwa kwenye sherehe zao.
Lakini Xavi amesema kwanini alifanya vile.
Kwenye maelezo yake alisema hivi, “Pale ndani ya basi tukiendelea kusherekea walijaribu kunisukuma wakati nikiwa kwenye pembe ya basi. Wakiendelea kufanya hivyo walikuwa wanajaribu kunivua viatu. Unaweza kunywa bia lakini inabidi usiende juu zaidi ukapitiliza. Bus parade ni sehemu ya mashabiki kufurahia na sio vinginevyo.”
Kinachoonekana hapa ulikua ni utani ambao Xavi aliona umepitiliza na ukamshinda.Kama video ilikupita ni hii hapa.
0 comments:
Post a Comment