Mchezaji bora wa msimu wa Arsenal, Alexis Sanchez jana alikuwa kwenye kiwango cha juu akiichezea Chile iliyoshinda 2-0 dhidi ya Ecuador katika mechi ya ufunguzi ya kundi A ya Copa America.
Sanchez hakufunga, lakini alipiga pasi murua ya mwisho iliyozaa goli la Eduardo Vargas.
Kipindi cha pili alionesha vitu vya hatari kwenye boksi la Ecuador ingawa hakufunga, lakini alionesha jinsi gani ni mtu wa cheche na hazuiliki kirahisi.
Tazama video ya chini ikionesha utamu wa Sanchez jana....
0 comments:
Post a Comment