Manchester United wanafikiria kutuma ofa Tottenham wakiomba kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya taifa ya England, Harry Kane, kwa mujibu wa Sky Sports.
Wakati huu Brand ya klabu hiyo ikiwa imefikia thamani ya Dola bilioni 1, Mashetani wekundu wako tayari kutumia kiasi chochoye cha fedha ili kupata wachezaji watakaoirudisha klabu nafasi za juu msimu ujao wa ligi kuu England.
Man United wapo sokoni kutafuta mshambuliaji baada ya kuachana na mpango wa kumnunua Radamel Falcao, wakati huo huo maisha ya baadaye ya Robin van Persie yakiwa shakani.
Harry Kane aligeuka lulu msimu uliopita akiifungia Spurs magoli 21 na alishinda tuzo ya PFA ya mchezaji bora kijana wa mwaka.
Nyota huyo tayari ameshaeleza kufurahia maisha White Hart Lane na haoni haja ya kuihama Tottenham, ingawa timu kubwa zinaweza kuishawishi klabu.
Kama dili hilo la kijana huyo mwenye miaka 21 litakamilika,Harry Kane ataungana na Teddy Sheringham, Dimitar Berbatov na Michael Carrick waliohama kutoka White Hart Lane kwenda Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment