Adebayor hajaIsaidia klabu yake ya Tottenham kwenye msimu ulioisha kwa kiasi kilichotegemewa ukilinganisha na mshahara wake mkubwa wa £100,000 kwa wiki.
Adebayor licha ya kuweka wazi kwamba bado anataka kurudi kwenye club ya Spurs na kuonyesha uwezo wake. Klabu hiyo bado ipo katika mpango wa kumuuza mchezaji huyo kutokana na gharama za mkataba wake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Adebayor aliposti picha akipiga saluti na kuandika “Feeling really fresh after my goal. Can’t wait to come back to Tottenham and show everyone the passion I have for the club. Looking forward to pre season! #COYS” akimaanisha kwamba najihisi ni mwenye furaha baada ya kufunga goli. Nasubiri kwa hamu kubwa kurejea klabu yangu ya Tottenham na kumuonyesha kila mmoja morali niliyonayo juu ya klabu yangu. Sasa kilichobaki ni muda wa maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa ligi!#COYS
Spurs bado wanatafakari juu ya klabu gani itakayokubali kumchukua Adebayor ukilinganisha na kiwango alichokionesha msimu uliopita huku ikiwa imebaki takribani miezi 12 tu ili mkataba wake uweze kumalizika klabuni hapo.
0 comments:
Post a Comment