Thursday, June 11, 2015

Mjumbe wa kamati ya Utendaji TFF, Geofrey Nyange 'Kaburu'.

KIKOSI cha wachezaji 23 wa Taifa Stars wanaoendelea na mazoezi mjini Addis Ababa nchini Ethiopia walikoweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.wanatarajia kuelekea Alexandria Misri kesho jioni.
Kocha Mart Nooij amesema  kabla ya kuondoka kuwa watatumia kambi ya Ethiopia kujiandaa kwa mchezo wa ugenini dhidi ya Misri na wachezaji wapo katika hali nzuri na wameahidi kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo.
Mchezo kati ya Misri na Tanzania unatarajiwa kuchezwa Juni 14, Uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria, ikiwa ni mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (Afcon) mwaka 2017.
Kikosi cha Stars kilichoko nchini Ethiopia ni Deogratias Munish, Aishi Manula, Mwadini Ali, walinzi Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Aggrey Morris, Mwinyi Haji, Salum Mbonde na Juma Abdul.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, Salum Telela, Frank Domayo, Jonas Mkude, Said Ndemla, washambuliaji Saimon Msuva, John Bocco, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, Mrisho Ngasa na Juma Liuzio.
Msafara wa Taifa Stars unaongozwa na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Vedastus Lufano na Geofrey Irick Nyange ‘Kaburu’.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video