Kikosi cha
timu ya taifa ya Uingereza maarufu kama ‘Simba watatu’ kiko katika maandalizi
yake ya mwisho kuikabili timu ya taifa ya Slovenia katika mchezo wa kufuzu
fainali za mataifa ya Ulaya Euro 2016, huku mshambuliaji nyota na nahodha wa
timu hiyo Wayne Rooney akikaribia kuvunja rekodi ya ufungaji bora wa timu hiyo.
Katika
mchezo huo utakao fanyika siku ya jumapili, Uingereza wanaongoza kundi wakiwa
na pointi 15 katika michezo 5 waliyocheza kwa maana ya kushinda michezo yao
yote ya awali, hawana majeruhi na wanatarajia kushinda katika mchezo huo
kujiongezea nafasi ya kufuzu mapema iwezekanavyo.
Lakini
kuelekea mchezo huo, mshambuliaji na nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney ‘Wazza’
ndio stori kubwa kutokana na ukweli kwamba amebakiza magoli mawili tu, kuifikia
rekodi ya ufungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya nchi hiyo
inayoshikiliwa na mkongwe Bob Chalton.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 29 hivi sasa, ameifungia Uingereza magoli 47 hadi
sasa, huku Bob Chalton akiwa amefunga magoli 49.
Rooney na
Bob Chalton wamejikuta katika hali hiyo hata katika ngazi ya klabu ambapo pia
Chalton ndiye mfungaji bora wa klabu ya Manchester United huku Wayne Rooney
‘Shreak’ akiikaribia kwa ukaribu rekodi hiyo.
Kuna uwezekano
mkubwa sana kwa Rooney kuzivunja rekodi hizo zote mbili kutokana na ukweli
kwamba bado ana miaka kadhaa mbele ya kufanya vizuri katika klabu na taifa.
0 comments:
Post a Comment