Friday, June 12, 2015


Mabingwa wa kihistoria nchini Ujerumani, Bayern Munich watakuwa tayari kumuuza kiungo wao mwenye uzoefu mkubwa na nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani,  Bastian Schweinsteiger kama tu kiungo huyo atahitaji kuondoka.

Bastian mwenye umri wa miaka 31 hivi sasa amekuwa akihusishwa na kuihama klabu hiyo tangu kutua kwa kocha Mhispania Pep Guardiola.

Manchester United wameripotiwa mara kadhaa kuhitaji saini ya kiungo huyo ambaye aliwahi kufanya kazi kwa mafanikio makubwa na kocha wa sasa wa Manchester United, Louis Van Gaal.

Nafasi ya kiungo huyo inaonekana mashakani katika kikosi hicho cha Pep Guardiola kutokana na uwepo wa kiungo Thiago Alcantara ambaye ni kipenzi cha Guadiola huku akionekana kuuweza mfumo wa tik-taka unaofundishwa na kocha huyo.

Aidha Xabi Alonso naye anafanya umuhimu wa mchezaji huyo kupungua.


Lakini mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo ya Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amesema kiungo huyo hajaonesha dalili zozote za kutaka kuondoka.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video