MABINGWA wa kandanda Tanzania bara, Dar Young Africans baada
ya safari ndefu ya msimu wa 2014/2015 wenye mafanikio kwao, kesho wanakabidhiwa
rasmi kombe la ligi kuu.
Yanga watakuwa wageni wa Azam fc katika mechi ya ligi kuu
itayopigwa kesho uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam dhidi ya waliokuwa mabingwa
msimu uliopita Azam fc.
Kaimu mgurugenzi wa bodi ya ligi kuu Tanzania bara (TPLB), Fatuma
Abdallah amethiubitisha Yanga kukabidhiwa kombe kesho katika uwanja wao wa
nyumbani.
“Kesho tunawakabidhi Yanga kombe katika uwanja wao wa
nyumbani, tumeshakamilisha taratibu zote kushirikiana na wadhamini Vodacom, na
wao kuna vitu watatoa kesho, lakini zawadi nyingine zitafanyiwa utaratibu
mwingine”. Amesema Fatuma.
Kwa upande mwingine, Fatuma amesema bodi ya ligi
wameridhishwa na ushindani uliopo kwenye ligi kuu mwaka huu akitumia kigezo cha
timu nyingi kufanana pointi mpaka dakika hizi za majeruhi.
“Mpaka sasa ni Polisi Morogoro ndio wanaoonekana wanashuka
daraja, timu nyingine hazijulikani mpaka sasa. Nyingi zimefungana pointi na
zinasubiri mechi za mwisho mei 9 kuamua nani anabaki nani anashuka, hakika ligi
hii imekuwa na ushindani mkubwa”. Amefafanua Fatuma.
Kuthibitisha kauli ya Fatuma, angalia msimamo wa ligi kuu
chini mpaka sasa:
Standings
Rnk | Team | MP | W | D | L | GF | GA | +/- | Pts | |||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Young Africans | 24 | 17 | 4 | 3 | 51 | 15 | 36 | 55 | |||
2 | Azam | 24 | 12 | 9 | 3 | 34 | 17 | 17 | 45 | |||
3 | Simba SC | 25 | 12 | 8 | 5 | 36 | 18 | 18 | 44 | |||
4 | Mtibwa Sugar | 25 | 7 | 10 | 8 | 24 | 24 | 0 | 31 | |||
5 | Mbeya City | 25 | 7 | 10 | 8 | 21 | 22 | -1 | 31 | |||
6 | Kagera Sugar | 25 | 8 | 7 | 10 | 22 | 26 | -4 | 31 | |||
7 | JKT Ruvu | 25 | 8 | 7 | 10 | 19 | 23 | -4 | 31 | |||
8 | Coastal Union | 25 | 7 | 10 | 8 | 19 | 24 | -5 | 31 | |||
9 | Ruvu Shooting | 25 | 7 | 8 | 10 | 16 | 28 | -12 | 29 | |||
10 | Tanzania Prisons | 25 | 5 | 13 | 7 | 18 | 22 | -4 | 28 | |||
11 | Ndanda | 25 | 7 | 7 | 11 | 20 | 29 | -9 | 28 | |||
12 | Mgambo JKT | 25 | 8 | 4 | 13 | 18 | 28 | -10 | 28 | |||
13 | Stand United | 25 | 7 | 7 | 11 | 22 | 34 | -12 | 28 | |||
14 | Polisi Morogoro | 25 | 5 | 10 | 10 | 16 | 26 | -10 | 25 |
0 comments:
Post a Comment