MSHAMBULIAJI hatari, Emmanuel Anord Okwi, raia wa Uganda, ameendelea
kuguswa na sapoti kubwa anayopewa na wachezaji, viongozi, benchi la ufundi na
mashabiki wa klabu ya Simba.
Okwi amekuwa akibanwa sana na mabeki wa timu pinzani kwasasa
kutokana na kutotabirika akiwa uwanjani na ni vigumu kujua atafunga muda gani
kwani ni mbunifu na mjanja wa kupiga mashuti ya kushitukiza.
Makipa kadhaa wakiwemo Mwadini Ali wa Azam na Ally Mustafa
wa Yanga wameshaonja joto la jiwe kutokana na magoli ya uwezo binafsi ya Okwi
walipokutana katika mechi za ligi kuu ambapo Simba ilitoka sare ya 1-1 na Azam
na machi 8 mwaka huu walishinda 1-0 dhidi ya Yanga.
Baada ya mechi ya mwishoni
mwa juma hili dhidi ya Azam fc ambapo Simba walishinda 2-1, Okwi alisubiriwa
kwa hamu na mashabiki wa Simba nje ya mlango wa ndani wa kuingilia uwanjani.
Okwi (kushoto) akijaribu kuchuana na Aggrey Morris wa Azam juzi uwanja wa Taifa
Nyota huyo alikuwa wa mwisho mwisho kutoka katika vyumba vya
kubadilishia nguo akifuatana na Waganda wenzake, Joseph Owino, Juuko Mursheed,
Simon Sserunkuma na Danny Sserunkuma.
Walipofika nje walikuta kuna umati wa mashabiki ilipopaki
basi ya Simba, yeye na wenzake wakaamua kupita njia nyingine, wakati anajaribu
kufanya hivyo kuna jamaa mmoja (jina halikufahamika kwa haraka) alimfuata Okwi
na kumwambia unaona watu wale! Wapo pale kwa ajili yako, nenda kawasalimie.
Wachezaji wenzake wakamkataza, lakini Okwi akaona ni busara
kwenda kuwatimizia haja yao, akatoa simu, wallet yake na kumkabidhi Owino na
kwenda kuwasalimia.
Baada ya kufika pale walimshangilia mno na kumkumbatia
wakionesha kuridhishwa na uchezaji wa ‘mfalme’ huyo wa Msimbazi.
Mtandao huu ukamuuliza Okwi anajisikiaje kupendwa kiasi
hicho, naye akajibu;
“Kwanza Simba ni nyumbani, hii ni sehemu ninayoishi kwa
furaha, licha ya changamoto ninazopata nikiwa uwanjani (kukamiwa na mabeki),
bado Wanasimba wamekuwa nami muda wote, hali hii inanifanya nijitume mazoezini
ili niendelee kufanya vizuri”.
“Makocha wangu, mashabiki wote, wachezaji wamekuwa upande wangu,
nina furaha mno ndani ya klabu hii iliyonipa heshima kubwa. Nawapenda Wanasimba
wote”.
Mpaka sasa Okwi amefunga magoli 11, mabao 6 nyuma ya kinara
Simon Msuva.
0 comments:
Post a Comment