Mchezo wa ufunguzi uliochezwa saa 7:00 mchana kwa kuzikutanisha timu za Dar Stars dhidi ya Mogadishu City ya Somalia (kwa upande wa wanaume), timu ya Dar Star walifanikiwa kuibuka na ushindi wa vikapu 112 kwa vikapu 46 vya Mogadishu City.
Mchezo mwingine kwa upande wa wanawake ulipigwa saa 9:00 alasiri ambapo Dar Stars ilichuana na Kampala City (KCCA), mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulimalizika kwa Kampala City kujinyakulia ushindi wa jumla ya vikapu 76 dhidi ya vikapu 61 vya Dar Stars.
Mchezo wa tatu ulikuwa unatarajiwa kuanza saa 12:00 jioni kwa kuzikutanisha timu za Dar City dhidi ya Qardo (wanaume) lakini mchezo huo ulichelewa kuanza na badala yake ukaanza saa 1:30 usiku kutokana na kukatika kwa umeme na kukosekana kwa mbinu nyingine ya kufanikisha mchezo huo kupigwa kwa muda uliokuwa umepangwa.
Mchezo huo uliokuwa mkali na kuvuta hisia za mashabiki wengi, ulimalizika kwa timu ya Qardo kuibuka na ushindi wa vikapu 85 wakati Dar City wao walimaliza wakiwa wamefunga vikapu 76.
Mchezo
wa kufunga dimba kwa siku ya leo ambao ulitarajiwa kuanza majira ya saa 2:00
usiku ambapo Cairo ingechuana na Mbeya (wanaume), umeanza saa 3:45 usiku na
hiyo ni kutokana na kukatika kwa umeme kulikopelekea kuvurugika kwa ratiba
hiyo. Tutakujuza matokeo ya mchezo huo mara baada ya mchezo kumalizika.
Michezo
ambayo inatarajiwa kuendelea kesho itakua ni kati ya Qardo dhidi ya Tanga
(wanaume), wakati Dar City itachuana dhidi ya Nairobi (wanawake), mchezo
mwingine utawakutanisha Dar Stars watakaochuana na Mbeya huku mcezo wa mwisho
kwa siku ya kesho ukiwa ni kati ya Mogadishu City dhidi ya Cairo (wanaume).
0 comments:
Post a Comment