Wachezaji wa Sevilla wakishangilia baada ya kipyenga cha mwisho.
HATIMAYE Sevilla wameibuka mabingwa wa ligi ya Europa baada ya kupata ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Dnipro katika mechi ya fainali iliyomalizika usiku huu National Stadium, Warsaw.
Mapema dakika ya 7' Dnipro waliandika bao la kuongoza kupitia kwa Nikola Kalinic, lakini dakika ya 28' Grzegorz Krychowiak akaisawazishia Sevilla.
Dakika ya 31' Carlos Bacca akaifungia Sevilla goli la pili, lakini Ruslan Rotan akaisawazishia Dnipro dakika ya 44'.
Carlos Bacca ndiye aliyeibuka shujaa baada ya kufunga goli la tatu na la ushindi kwa Sevilla katika dakika ya 73'.
0 comments:
Post a Comment