Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Azam FC itaiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo inayofanyika Dar es Salaam mwaka huu ikiwa ni bingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2013/14.'
BAADA ya kufanikiwa kumrejesha kocha mkuu Muingereza Stewart John Hall, kikosi cha Azam kitaingia kambini jijini Dar es Salaam Juni 15 kujiandaa kwa ajili ya michuano ya Kombe la Kagame.
Michuano ya Kombe loa Kagame inayoshirikisha Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, itafanyika jijini hapa Julai mwaka huu.
Jaffar Idd Maganga, msemaji wa Azam FC, amesema kikosi chao kitaingia kambini Juni 15 ikiwa ni siku saba baada ya makocha wao wapya kuripoti kutoka Uingereza.
0 comments:
Post a Comment