Wednesday, May 27, 2015

BAADA ya Shirikisho la soka Tanzania TFF kushindwa kumtimua kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij,  mwenyekiti wa zamani wa Simba na Mbunge wa sasa wa Tabora mjini, Alhaj Ismail Aden Rage amelivalia njuga suala hilo na kuahidi kulipeleka kwenye mkutano wa Bajeti wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Bunge la Bajeti linaendelea mjini Dodoma, lakini bado wizara inayohusika na michezo haijawasilisha mbele ya Wabunge. 
"Wakati wa kikao cha bajeti nitamuomba Waziri (Dr. Fenella Mukangara) amtimue huyo kocha hata ikibidi kwa kutoa shilingi". Amesema Rage na kusisitiza: "kocha huyo (Nooij) hana faida kwetu. Utaratibu duniani kote ni kwamba kocha yeyote anapofanya vibaya anafukuzwa, si umeona Real Madrid walivyomfukuza Carlo Ancelotti?"
Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij
"Michezo 18 anafungwa michezo 13, unataka apewa muda gani ? mimi natoa hoja, kocha aondoke haraka sana. Tunahitaji makocha wazalendo ambao wameiletea sifa nchi hii, sisi tulichukua kombe la Cecafa tukiwa na makocha wawili wazalendo kule Mwanza, marehemu Kinanda na Charles Boniface".
"Abdallah Kibadeni ndiye kocha aliyeifikisha Simba fainali ya kombe la CAF 1993, kwanini tunawadharau makocha wetu wa kizalendo?". Amehoji Rage.
"Marehemu Mziray ndiye aliyechukua Challenge Cup kule Nairobi, nani amechukua kombe nje ya nchi tangu Mziray afariki?. Sikubaliani na huyo kocha, maoni yangu ni kwamba atimuliwa halafu tuangalie makocha wazawa".

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video