Wakati makocha
wanapofukuzwa, hasa hasa kwenye klabu kubwa, mara nyingi huwa tunaligeuza kuwa
jambo la uadilifu. Tunawaonea huruma (au hapana) na huwa tunajiuliza kama
walistahili kufukuzwa au walifanya kila kilichotakiwa ili kulinda vibarua vyao.
Tunatumia vipimo vyetu kupima hivi – matokeo, ukubwa wa bidhaa (image), aina ya
uchezaji – tunajitahidi kuwa na usawa kwa kuangalia sababu zingine
zilizopunguza ubora kama: majeruhi, muda, rasilimali, uwezo wa kuongoza na
maono ya mbali na mahusiano binafsi.
Mengi
tuliyokwishayataja yanaingia katika uamuzi wa Real Madrid kumfukuza Carlo
Ancelotti. Kwa vyovyote vile – iwe ni wachezaji au mashabiki – wengi walitaka
aendelee kuwepo na waliamini juu ya kile alichokuwa anakifanya.
Kwa
nini walitaka asiondoke?
Kwa wachezaji , labda
sababu kubwa inaweza kuwa walipenda kufanya kazi chini yake. Aliwachukulia kama
watu wazima. Alikuwa mtetezi wao kwa umma. Tofauti na wengine waliomtangulia,
hakukuwa na mkanganyiko wowote iwe ni sehemu ya kufanyia mahojiano, uwanja
wa mazoezi au vyumba vya kubadililshia
nguo wakati Ancelotti akiongoza.
Kwa mashabiki, itakuwa
ni vile alivyoiwakilisha klabu yao, bila ya kuwapa shutuma waamuzi au klabu
nyingine na kuwa mtazamo chanya muda wote, pamoja na sababu kubwa ya kuwaletea
mataji manne ndani ya misimu miwili hii ikijumuisha taji lililongojewa kwa muda
mrefu la Ligi ya Mabingwa. Sababu nyingine ambayo ni halisi sana, ni kuwa
katika makocha wote 46 walioifundisha Real Madrid katika miaka 113 yake katika
historia hakuna mwenye uwiano mkubwa wa kushinda kumzidi Carlo Ancelotti.
Lakini kanuni za
kumbakiza (au kumwondoa) kocha zinabaki kuwa rahisi. Hautakiwi kuwa na huruma,
kama ukiamua.
Je, kuna mtu yeyote
ambaye tunadhani ataweza kufanya kazi nzuri zaidi? (inaweza kuwa kwa sababu ya
matokeo, aina ya uchezaji, utambulisho, gharama au vingine)
Florentino Perez ni
Rais wa Real Madrid, hiyo ndio kazi yake. Kama atafikiri mtu mwingine anaweza
kufanya kazi nzuri zaidi, basi anaweza kuamua kufanya lolote.
Kitu alichofanikiwa
kushinda Ancelotti (au kocha mwingine yeyote) hapo nyuma, inaweza kutumika
kuona nini timu yake inaweza kushinda hapo baadae. Lakini kuna usemi usemao,
“Uwezo wako wa jana, sio mafanikio ya kesho”
Florentino atazungumziwa
zaidi kwenye maamuzi yake ya kumuondoa Ancelotti,na kumweka kama ni Benitez au kocha wa Sevilla, Unai
Emery au mtu mwingine. Baadae, watu watalinganisha mafanikio ya kocha atakayekuja
baada ya Ancelotti. Rahisi hivyo.
Nadhani Florentino na
bodi yake hapa wamechemka vibaya, na yeyote yule watakayemchagua, ukizingatia
wanafanya mageuzi makubwa ya ghafla, hii itaifanya klabu kurudi nyuma. Muda
utaongea.
Lakini tujikumbushe ni
kwa nini Perez anafanya maamuzi kama haya kwenye moja ya vilabu vikubwa kabisa duniani.
Yeye haimiliki Real Madrid; ni mtu
aliyechaguliwa kuwa Rais, uchaguzi wa hivi karibuni ni ule wa Juni 2013,
alipokuwa hana mpinzani.
Kwa nini alikuwa hana
mpinzani? Vizuri sababu moja inaweza kuwa, ni vizuri kwa wanachama wa Real
Madrid wanapata nafasi ya kumchagua Rais ambaye ataweza kusimamia mipango yao
na kila kitu, pili siku hizi uchaguzi wao si wa kidemokrasia sana.
Mwaka 2012, bodi ya
klabu (ikiongozwa na Perez) ilivipitia tena vipengele vya kusimama kugombea
urais wa klabu. Aliongeza muda wa kipengele cha umri wa uanachama kutoka miaka 15 hadi kufikia 20,
lakini pia mgombea atatakiwa kuonesha kwamba ameweka benki au amepata udhamini
wa benki ulio sawa na asilimia 15 ya bajeti ya mwaka. Kwa mwaka 2013, ilikuwa
Dola 83 Mil; kufikia uchaguzi ujao inatarajiwa itakuwa kama Dola 120 Milioni.
Hii inamaanisha nafasi
ya wagombea wengine kujitokeza kutangaza nia, inaendelea kuwa finyu. Perez ni
moja ya watu matajiri sana Spain; anaendesha makampuni makubwa sana (yenye
thamani ya mabilioni ya dola) ya ujenzi, akipiga mluzi tu, anajikuta
amezungukwa na watu wa benki wakimwahidi udhamini wa vitu vingi. Ni ukweli
usiopingika katika dunia ya leo si watu wengi wanaoweza kuiomba benki iwape
udhamini wa Dola 120 Mil na huku wakiwa ni wanachama wa Real Madrid kwa miaka
20 ili waweze kugombea urais wa Real Madrid. Unaweza kuwahesabu kwa kutumia
vidole vya mikono yako miwili.
Rais wa zamani kabla ya
Perez, Ramon Calderon, aliwahi kutania kuwa, njia nzuri ya yeye kujihakikishia
urais ni kuongeza kipengele kingine kitakachosema, wale wote ambao majina yao
yanaanza na herufi “F-l-o” ndio wanaweza kugombea.
Wale wanaomsapoti Perez
watasema kwamba sheria hizi hazikutengenezwa ili yeye pekee aweze kutawala Real
Madrid. Bali, zinatumika ili kuilinda klabu na wale wasio na ubora, watu ambao
wanaweza kuchezea hela za watu wengine katika mambo yao ya ajabu ajabu. Kama
unahitaji watu maarufu na matajiri ndio wawe marais, basi hawatahitaji kuitumia
Real Madrid kuwa kama chombo cha usafiri kupata utajiri.
Wakati mijadala ikiendelea,
inazidi kuwa ya ajabu. Sio kwa sababu tu, urais ni zana yenye thamani kwa watu
maarufu na kutengeneza mtandao hata kwa matajiri lakini sababu kubwa ni kuwa
inaondoa watu wengi wenye vipaji, akili na wanaoangalia mbele kushika wadhifa
huo katika klabu.
Unapokuwa katika chombo
cha ndani kabisa cha uongozi na unaona kabisa kwamba kiongozi huyo anaenda
kuongoza kwa muda mrefu kweli, kwa
uhalisia kabisa hii hufifiza ile hali ya mawazo kukinzana na kumpinga kiongozi
huyo. Pale mambo yanapoenda mrama, basi hapo mtajichunguza wenyewe na hitimisho
litakuwa lile lile kila siku: tulikuwa sahihi, hatukuwa na njia nyingine, ni
bahati mbaya.
Tangu amfukuze Vicente
Del Bosque mwaka 2013, Florentino amekuwa na vipindi viwili tofauti kama Rais
na jumla ya makocha tofauti nane. Nini anacho cha kutuonesha? Kombe moja la La
Liga na Kombe moja la Mfalme chini ya Mourinho na Kombe moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe moja
la Mfalme, Super cup moja ya UEFA na Kombe moja la klabu bingwa ya Dunia chini
ya Ancelotti. Iko hivyo.
Katika taasisi ya
kawaida – ile ambayo bosi mkubwa hajagundishwa kwenye kiti chake na ambayo
mawazo tofauti yanakaribishwa kama chachu ya kuzidi kusonga mbele na kufanya vema – unaweza kuhitimisha kwa
kusema kuna kitu hakipo sawa hapa.
Mtazamo nao ni tatizo. Wenyewe
wanadhani labda mtu mwingine anaweza kufanya vizuri katika klabu hii kuliko
Ancelotti. Tutaona tu. Kitu ambacho kwa asilimia kubwa, hatutakiona – hata kama
haimiliki klabu na hata kama klabu ndio inayosimamia chaguzi -- kuna mtu
anaweza kufanya kazi nzuri na klabu kuliko Florentino.
0 comments:
Post a Comment