JUVENTUS wamewandika mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa ulaya, Real Madrid magoli 2-1 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Uropa iliyopigwa Uwanja wa Juventus, mjini Turin.
Mapema dakika ya 9' kipindi cha kwanza, Alvaro Morata aliwafungia Juventus goli la kuongoza akimalizia pasi ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Carlos Tevez.
Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo alipigiwa pasi murua na James Rodriguez dakika ya 27' na kuisawazishia Real goli hilo.
Carlos Tevez aliifunga Juventus goli la pili kwa mkwaju wa pebalti dakika ya 58'.
Kwa matokeo hayo Juventus wanahitaji sare ya aina yoyote ile Santiago Bernabeu ili kusonga mbele moja kwa moja, wakati Real wanahitaji ushindi wa goli 1-0 ili wasonge mbele kwa faida ya goli la ugenini.
Takwimu za mchezo huo zinaonesha kuwa Real Madrid wamemiliki mpira kwa asilimia 53 kwa 47 za Juventus.
Kesho Barcelona wanaikaribisha Bayern Munich katika mechi ya nusu fainali uwanja wa Camp Nou.
statistics :
7
shots on target
3
4
shots off target
7
47
possession (%)
53
1
corners
5
3
offsides
1
20
fouls
13
4
yellow cards
3
12
goal kicks
6
3
treatments
0 comments:
Post a Comment