Mechi ya kwanza uwanja wa Taifa, Yanga na Ndanda fc zilitoka suluhu pacha ya bila kufungana.
YANGA SC wamepigwa mkwara na Ndanda fc wenye uchu wa kuvuna pointi
tatu za mwisho na kubakia ligi kuu.
Mpaka sasa Ndanda fc wapo kwenye hatari ya kushuka daraja
wakijikusanyia pointi 28 katika nafasi ya 11, sawa na Tanzania Prisons, Mgambo
JKT, Stand United wenye idadi ya pointi hizo na timu zote zimebakiwa na mchezo mmoja
tu kumaliza msimu huu mgumu wa ligi kuu.
Kocha mkuu wa Ndanda fc, Meja Mstaafu, Abdul Mingange
amesema wamejiandaa vilivyo kupambana na Yanga mei 9 mwaka huu uwanja wa
Nangwanda Sijaona, Mtwara na kuvuna pointi tatu muhimu.
“Sisi tutapambana mpaka tone la mwisho, Yanga ni timu bora
na Mabingwa, lakini kwenye mpira lolote linaweza kutokea. Waje wakijua Ndanda
inaska pointi tatu na imejipanga kuzipata”. Amesema Mingange na kuongeza: “Tunalingana
pointi na timu tatu katika msimamo (pointi 28), hapo kila mtu anaweza kushuka
daraja, tunafahamu ugumu wa mechi ya jumamosi, lakini tuko tayari nakwambia!”.
0 comments:
Post a Comment