KIMAHESABU watu wengi wameshaishusha daraja Polisi Morogoro
msimu huu kutokana na kuwa na pointi 25 tu katika msimamo baada ya kucheza
mechi 25.
Mechi ya mwisho mei 9 mwaka huu, Polisi watachuana na Mbeya
City katika uwanja wa Sokoine Mbeya na mechi hiyo itaamua hatima ya Maafande
hao wanaopumulia mashine.
Lakini kuna kitu kinasahaulika ambacho ni tofauti ya magoli
ya kufunga na kufungwa.
Mpaka sasa Polisi wapo mkiani wakiwa wamefunga magoli 16 na
kufungwa 26, tofauti ya magoli ni -10.
Stand United wenye pointi 28 katika nafasi ya 13 wamefunga
magoli 22 na kufungwa 34, tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni -12.
Mgambo JKT waliopo katika nafasi ya 12 na pointi 28 wamefunga magoli 18 na kufungwa 28, tofauti ya
magoli ya kufunga ni -10 sawa na Polisi Morogoro.
Maana yake kama Mgambo watafungwa na Azam fc 1-0 mei 9 mwaka
huu, Polisi akashinda 1-0 dhidi ya Mbeya City atakuwa na magoli 17 ya kufunga
na 26 ya kufungwa, tofauti itakuwa -9 na watawazidi Mgambo watakaokuwa na
wastani wa -11. Maana yake Mgambo watashuka daraja kwasababu Polisi watafikisha
pointi 28, na Mgambo 28, lakini Polisi watakuwa juu kwa tofauti ya magoli.
Kama Stand watafungwa na Ruvu Shooting mei 9 mwaka huu
watakuwa na magoli 12 ya kufungwa na 35 ya kufungwa, tofauti itakuwa -13. Kwa
maana hiyo Stand na Mgambo watakuwa chini ya Polisi kama wataifunga Mbeya City.
Ndanda fc wana pointi 28 mpaka sasa katika nafasi ya 12.
Wamefunga magoli 20 na kufungwa magoli 29, tofauti ni -9. Endapo watapata sare
siku ya mwisho dhidi ya Yanga, matokeo mengine yakatokea kama nilivyoeleza hapo
juu, maana yake Mgambo JKT na Stand United watakuwa wameshuka daraja.
Tanzania Prisons wamebakiza mechi moja dhidi ya Kagera
Sugar, lakini kwasasa wapo nafasi ya 10 kwa pointi zao 28. Kitu kizuri ni
kwamba wamefunga magoli 18 na kufungwa 22, tofauti ni -4. Huu ni wastani mzuri
ukilinganisha na timu za chini yake.
Kama atafungwa 1-0, atakuwa amefunga magoki 18 na kufungwa
23, tofauti itakuwa -5. Wastani ambao utamsaidia kama matokeo mengine yatatokea
kama nilivyoeleza hapo juu.
Kwa mahesabu hayo, bado Polisi Morogoro
hawajashuka daraja, cha msingi washinde mechi ya mwisho, halafu wasikilizie
kwingine kutakuwa na matokeo ya aina gani. Huu ni mpira wa miguu, matokeo mpaka
dakika 90’ zikamilike.
0 comments:
Post a Comment