Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Ndanda FC iliishika Yanga kwa suluhu katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa."
ABDUL Mingange, kocha mkuu wa Ndanda FC, ataiongoza timu hiyo katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu dhidi ya Yanga akiwa hospitalini, imefahamika.
Ndanda FC, timu pekee VPL kutoka mkoani Mtwara, itakuwa na kibarua kigumu mbele ya mabingwa Yanga katika mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kesho jioni.
Mingange, meja mstaafu, ameuambia mtandao huu muda mfupi uliopita kuwa hatakuwapo uwanjani kesho kuingoza timu yake katika mechi hiyo muhimu kutokana na matatizo ya kifamilia yanayomkabili.
"Kwa sasa niko Dar es Salaam, tena hospitali ninamuuguza mmoja wa wanafamilia. Kila kitu kinakwenda vizuri katika timu maana ninawasiliana na viongozi na makocha wenzangu kuhakikisha timu inafanya vizuri dhidi ya Yanga kesho.
"Kesho ndiyo pona na kufa yetu. Nitaendelea kutoa maelekezo ya nini kifanyike kuifunga Yanga. Tutacheza dhidi ya timu ngumu na yenye wachezaji wazuri na wazoefu.
"Kikubwa nimewaambia viongozi wahakikishe wachezaji wanacheza kwa nidhamu kubwa na wasiingie uwanjani wakiwa na hofu," amesema zaidi Mingange.
Kocha huyo alipewa jukumu la kuinoa Ndanda FC kutokana na kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu, Dennis Kitambi mwishoni mwa mwaka jana.
Ndanda imekusanya pointi 28 katika mechi 25 zilizopita sawa na Prisons, Stand United na Mgambo Shooting ambazo zinapumulia mashine kuukwepa mstari wa kuporomoka daraja msimu huu.
Timu mbili zitashuka daraja kesho kuzipisha timu tatu; Africans Sports ya Tanga, Mwadui FC ya Shinyanga na Majimaji ya Ruvuma.

0 comments:
Post a Comment