Tuesday, May 5, 2015

MLINDA mlango wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ amesema kutolewa na Etoile Du Sahel katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya 16 bora  ni bahati mbaya kwao kwani walicheza vizuri kwa kujiamini na kushambulia.
Yanga wametupwa nje na Etoile kwa ushindi wa jumla wa magoli 2-1 baada ya mechi ya awali kutoka sare ya 1-1 uwanja wa Taifa, Dar es salaam na kufungwa 1-0 mwishoni mwa juma lililopita nchini Tunisia.
 Dida amesema kuwa bao  lililowaondoa katika michuano hiyo lilitokea baada ya kujichanganya yeye na mabeki wake na kumkuta mchezaji wa Etoile ambaye alifunga kirahisi kwa kichwa.
“Kwanza tunamshukuru Mungu mazingira ya Mchezo yalikuwa mazuri. Tulipoteza mechi lakini hayakuwa matarajio yetu, upinzani ulikuwa mkubwa sana,' amesema Dida na kusisitiza: "Nina imani kuwa wametufunga kwa bahati mbaya lakini jitihada ambazo tulizionesha ni kubwa zaidi ambazo mtu yoyote akiona naamini atatupa moyo wa sisi kuendelea katika mchezo wetu wa ligi. Tumetoka kwa bahati mbaya sio kwamba tumeshindwa katika uwezo tulionao".

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video