Mshambuliaji wa klabu ya Swansea city raia wa nchini ufaransa BAFETIMBI GOMIS Kama alivyofanya Novemba 9 mwaka jana baada ya
kuifungia Swansea City Bao la ushindi dhidi ya Arsenal, Straika huyo ameiua tena Arsenal kwa kufunga Bao moja na pekee Uwanjani Emirates katika
Mechi ya Ligi Kuu England.
Novemba 9 mwaka jana, Bafetimbi Gomis alifunga
Bao la ushindi Dakika ya 78 kwenye Mechi ya Ligi ambayo Arsenal walilala 2-1 na
safari hii Straika huyo akitokea Benchi Dakika ya 74 akichukua nafasi ya mchezaji Ki Sung-yueng na
kuipa ushindi Swansea City kwa Bao la Dakika ya 85 ambalo Refa Kevin Friend
aliamua ni Bao kwa msaada mkubwa wa Teknolojia ya Mpira Kuvuka Mstari wa Goli,
baada ya Kipa wa Arsenal Ospina kuufuta Mpira uliokuwa ukielekea kugusa nyavu hapo jana.
Matokeo hayo sasa yamewaacha Arsenal
Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Man City na Pointi 2 mbele ya Man United
walio Nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi kuu soka nchini uingereza.
Mechi inayofuata Arsenal wataifuata Manchester United
Ugenini katika dimba la Old Trafford hapo Jumapili Mei 17.




0 comments:
Post a Comment