MFUNGAJI bora wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015, Simon Happygod Msuva
amesema mechi dhidi ya Simba ni rahisi, lakini wanafungwa kwasababu ya presha
kubwa kutoka kwa viongozi.
“Kila ikifika mechi na Simba, basi viongozi wanakuwa na
presha sana, wanaweka mipango mingi, wanatutaka kufanya mambo mengi ambayo
siwezi kuyataja, mchezaji unaingia uwanjani ukiwa na hofu ya kukosea, kweli
unakuta umekosea”. Amesema Msuva na kuongeza: “Mechi ya Mgambo na Yanga ni
ngumu kuliko ya Simba, lakini utani wa jadi ndio unasumbua, mechi ya Simba ni
ya lawama, kila mtu anaiangalia. Raha ya Yanga kuifunga Simba, hivyo mazingira
yanakuwa magumu kiuchezaji, lakini ni rahisi sana”.
Msuva amefanikiwa kufunga magoli 17 msimu uliopita ambao
umemalizika mei 9 mwaka huu kwa Yanga kufungwa goli 1-0 na Ndanda fc, lakini
tayari walikuwa wameshatangazwa mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Msuva hakujumuishwa katika kikosi cha Yanga dhidi ya Ndanda kwasababu alikuwa Afrika kusini kufanya majaribio katika klabu
ya Bidvest Wits inayoshiriki ligi kuu Afrika kusini.
Msuva amefuzu majaribio hayo na sasa anasubiri viongozi wa
Bidvest kutua nchini kuzungumza na Yanga ambao ana mkataba nao.

0 comments:
Post a Comment