Na Bertjha Lumala, Dar es Salaam
'Ajibu ndiye mchezaji wa kwanza kupiga 'hat-trick' VPL msimu huu.'
MSHAMBULIAJI Ibrahim Ajibu wa Simba, amesema amefurahi kufunga goli la pili kwa kichwa msimu huu lililoisaidia timu yake kuibuka na ushindi 2-1 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Taifa jana.
Mshambuliaji huyo aliyeaminika katika kikosi cha Mserbia Goran Kopunovic cha Simba, ndiye mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick msimu huu alipofunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Tanzania Prisons FC Uwanja wa Taifa Februari 28.
Goli lake la kwanza la kichwa msimu huu alilifunga katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Police MoroFC mjini Morogoro Februari 15.
"Nimefurahi kufunga bao langu la pili la kichwa msimu huu, ni goli zuri kwangu, lakini linatokana na jitihada za timu nzima kufanya mazoezi kwa nguvu," amesema Ajibu.
Nyota huyo aliyekulia Simba B, alipiga hat-trick pia katika mechi waliyoshinda 4-0 dhidi ya Taifa ya Jang'ombe visiwani Zanzibar Januari mwaka huu akiwa ni mchezaji wa pili kupiga hat-trick katika michuano ya Kombe la Mainduzi baada ya winga Simon Msuva wa Yanga kuipiga timu hiyo hiyo visiwani humo.
0 comments:
Post a Comment