Sunday, April 12, 2015


Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

YANGA SC na Mbeya City fc zimekutana katika mechi ya nne ya ligi kuu soka Tanzania bara tangu City wapande msimu uliopita.

Msimu uliopita, Yanga walitoka sare ya 1-1 uwanja wa Sokoine kabla ya kuwafunga Mbeya City bao 1-0 uwanja wa Taifa Dar es salaam.

Msimu huu mechi ya kwanza kule Mbeya, Yanga walishinda mabao 3-1 uwanja wa Sokoine na leo wametoa kipigo kama hicho uwanja wa Taifa.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Kpah Sherman, Salum Telela na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Bao la kufutia machozi la Mbeya City limefungwa na Themi Felix ‘Mnyama’.

Kwa matokeo haya, Yanga wameendelea kuwa wababe dhidi ya timu inayomilikiwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.

Matokeo ya leo yanawafanya Yanga wazidi kupaa zaidi kileleni wakijikusanyia pointi 46 baada ya kucheza mechi 21.

Nafasi ya pili inashikiliwa na mabingwa watetezi Azam fc wenye pointi 38 kufuatia kushuka dimbani mara 20 na hapo jana walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar uwanja wa Manungu, Turiani, Mkoani Morogoro.

RIPOTI YA MECHI

Yanga waliandika bao la kwanza dakika ya 8' kupitia kwa Kpah Sherman akimalizia krosi ya Oscar Joshua na kumzidi ujanja beki Juma Nyosso.

Dakika ya 37' Yanga waliandika bao la pili kupitia kwa Salum Telela aliyepiga shuti la chini chini akipokea mpira wa adhabu ulichongwa na Haruna Niyonzima na mpira kuwapita mabeki wa Mbeya City na kutinga nyavuni.

Dakika mbili baadaye, (dk 39'0)  Themi Felix aliifungia goli la kwanza  Mbeya City akipokea pasi ya Kenny Ally na kutulia kisha kuburuza mpira eneo la hatari na kumtazama kipa Ally Mustapha na kufunga goli zuri kwa ‘kuchipu’.

Dakika chache kabla ya kwenda mapumziko timu nzote mbili zilishambuliana kwa zamu, lakini mabeki wa timu zote walikuwa makini kuonoa hatari.

Hadi dakika 45 zinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa magoli 2-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, Yanga wakitengeneza nafasi kwa haraka.

Dakika ya 49' Nadir Haroub aliifungia Yanga goli la tatu kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Niyonzima

Dakika ya 53' Mbeya City walipata pigo kufuatia Them Felix kuoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na Mwamuzi Akrama baada ya kumchezea vibaya Salum Telela.

Kocha Juma Mwambusi alifanya mabadiliko dakika ya 59'  akiwatoa wachezaji wawili  ambapo  Deus Kaseke alikwenda benchi nafasi yake ikachukuliwa na Peter Mapunda, Raphael Alfa naye akaenda benchi nafasi yake ikachukuliwa na Yusuph Abdallah.

Dakika ya 61' Salum Telela alishindwa kuendelea na mchezo kutokana na madhambi aliyofanyiwa na Themi na nafasi yake ikachukuliwa na Hassan Dilunga.

Dakika ya 69' Tambwe alipiga kichwa akimalizia krosi ya Saimon Msuva, lakini mpira ukagonga mwamba wa kushoto kwa chini.

Dakika ya 70' Yanga walifanya mabadiliko, Sherman alikwenda benchi na nafasi yake ikachukuliwa na Mrisho Ngassa.

Dakika 10 za mwisho, timu zote zilishambuliana kwa zamu, lakini hakuna aliyekuwa na hesabu nzuri za kufunga goli.

REKODI ZA MAGOLI YALIYOFUNGWA LEO

Kpah Sherman amefunga goli la pili tangu atue Yanga, Goli lingine alifunga dhidi ya Coastal Union, Yanga wakishinda 8-0 jumatano ya wiki hii uwanja wa Taifa.

Salum Telela naye alifunga goli la kwanza msimu huu dhidi ya Coastal Union na leo amefunga goli la pili dhidi ya Mbeya City.

Bao la Themi Felix ni la tano msimu huu tangu ajiunge na Yanga kutoka kutoka Kagera Sugar.




0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video