Na Kassim Mtolea
Mtoa habari wa timu ya Ruvu Shooting kutoka kambi ya 832 Kj kambi ya Ruvu, Masai Bwire ameitabiria mabaya Yanga itakapokwenda Tunisia.
Akizungumza na MPENJA BLOG mara baada ya mchezo kati ya Yanga dhidi ya Etoile du sahel ya Tunisia uliomalizika kwa sare ya goli moja kwa moja,Bwire alisema kuwa Yanga haikuonesha makali yoyote dhidi ya waarabu hao.
"Hakuna kitu ndugu yangu, Yanga hakuna kitu alichokifanya leo(jana)pale taifa, wamecheza mpira mbovu kabisa, hawa jamaa na kama wakicheza hivi kule Tunisia watafungwa kumi mbili bila'.
"Wenzao wamecheza vizuri bwana ! Walikuwa wanatakata uwanjani kwao,walikuwa wanafanya kila wanachotaka mara watembee mara wakimbie walileta burudani sana hawa Watunisia .alisema Bwire.
Msemaji huyo pia amewataka Yanga kutokata tamaa na matokeo ya nyumbani hapa kikubwa ni kwenda kucheza soka la kuvutia huko ugenini.
Timu ya Yanga itakuwa na mlima mrefu kuupanda itakapo rudiana na Etoile kule nchini Tunisia kwani itahitaji ushindi wowote au sare ya magoli kuanzia mawili ili kusonga mbele.

0 comments:
Post a Comment