BAADA ya Yanga kutoa sare ya 1-1 dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 kombe la shirikisho uliopigwa jana uwanja wa Taifa Dar es salaam, Ukurasa wa Naipenda YANGA kwenye ukurasa wa facebook umetoa pongezi kwa vijana wa Yanga.
Ujumbe wenyewe soka hapa chini;
"Hatuna budi kuwapongeza vijana wetu kwa mchezo wa jana, ukiachana na matokeo kuna kitu cha ziada wamekionyesha kuwa kimepandwa na kinakua katika akili na miili yao ambacho kitapelekea kuja kuwa timu imara sana!
Sio sisi wala wao waliotegemea mchezo ungekuwa mgumu kiasi kile, Etoile du sahel walitawala kipindi cha kwanza tukawafunga nasi tukatawala kipindi cha pili tukafungwa!kwa mchezo wa jana hakuna mwenye uhakika kuwa timu fulani imesonga mbele japo asilimia kubwa wanazo ESS,mechi ya marudiano itakuwa ngumu kwa pande zote!kutoa upinzani mkubwa na kutawala mchezo dhidi ya timu kubwa kama ESS ni kitu ambacho wachezaji pamoja na benchi letu la ufundi wanahitaji pongezi ndio maana nadiriki kusema huu mchezo bado unahitaji dk 90 zingine kutegua kitendawili hiki.
Binafsi sababu hizi ndio zilipelekea tusipate matokeo chanya uwanja wa nyumbani.
Ubora , uimara na ukomavu wa kikosi cha Etoile, ukiachana na sababu zote hii ni ya kwanza ESS wanajua bana bila kupepesa macho au unazi hawa jamaa lazima wapewe sifa yao hii ni timu bora ambayo sio tishio kwa Yanga tu bali Afrika nzima ndio maana ni miongoni mwa vigogo wa Afrika!angalia muunganiko wao kutoka nyuma hadi mbele jinsi walivokuwa wanacheza mpira unafika mbele kwa malengo na pasi ambazo nyingi zilikuwa direct forwad iwe fupi ama ndefu!soka lao likichagizwa na stamina, miili mikubwa na vipaji vyao.
Pengo la Salum Telela, Kwa mara ya kwanza nagundua kumbe akikosekana mchezaji fulani kunakuwa na pengo kwa msimu huu katika kikosi chetu!timu ina rotation kubwa hii ilichangiwa na kikosi kikubwa tulichonacho, Hassan Dilunga alishindwa kuziba nafasi ya Salum Telela alizidiwa nguvu,akili yani kila kitu kuna muda akapotea kabisa,hapa ndipo ugonjwa wetu ulipokuwa!Mechi ya marudiano Salum Telela atakuwepo hii itachangia mechi kuwa ngumu.
Hali ya hewa, unapokuwa nyumbani unategemea kila kitu katika mazingira yako ikupendelee wewe!Wale jamaa adui yao ni Jua kali,ungewaona muda wote wanakunywa maji ,wakianguka anguka lakini hali ya hewa ikatusaliti kimvua kilinyesha na jua kupotea kabisa na kuwafanya jamaa wajihisi wapo kwao katika nyasi za Stade Olympique de Sousse mjini Sousse, Tunisia!na uwanja ulivo mzuri basi kila kitu walihisi wamekizoea.
Kuumia kwa key players,tumeshindwa kuwafanyia fitna nje ya uwanja tukiwa kwetu wao wametufanyia fitna ndani ya uwanja hapa hapa kwetu!Wachezaji wetu wengi usiku wa kuamkia leo watakuwa wamelala na barafu kupooza maumivu jinsi walivokuwa wanapigwa daruga chini chini pasipo kushtukiwa na kuonekana.Nadir Haroub, Juma Abdul walishindwa kuendelea na mchezo pia kuna baadhi waliendelea kucheza wakiwa na maumivu!hii ilipunguza ufanisi wa kikosi chetu.
Waamuzi wa mchezo huo wakiongozwa na Samwel Chirindiza akisaidiwa na rsenio Marenguka, Celio de Jesus Musabe, Jose Maria Bachide wote kutoka nchini Msumbiji kuna matukio uwanjani waliaamuru kwa kutuuma ikafikia kipindi mashabiki wakaanza kurusha makopo kuonesha kutoridhishwa na maamuzi yao.
Mbinu uwanjani, muda mwingi wapinzani wetu walicheza compact football hawakuacha kabisa nafasi za Ngassa wala Msuva waweze kukimbia!aina hii ya soka imekua inampa shida sana Msuva, walitubana tulipokuwa tunashambulia walifunguka wakipata mpira, mara nyingi wachezaji wetu walikamatwa offsides mara 8 huku wapinzani wetu offside ikiwa 1 tu!Ilikuwa inapigwa mipira ya juu kwenda kwa Ngassa ambaye alikuwa akikabana na jitu refu Bedui,mara zote mipira hiyo ilipotea.
Bado tuna nafasi ya kusonga mbele iwe kwa ushindi ama sare ya mabao zaidi ya 1, Kuna kitu kinaniambia katika nafsi yangu kuwa huko huko tutaenda kufanya maajabu japo haitakuwa kazi rahisi.
Hongera Ally Mustafa japo ulifungwa goli jepesi lakini uliweza kuokoa zaidi ya magoli 2 ya wazi.
SHIKAMOO DOGO SAID JUMA MAKAPU.
Asubuhi njema Wananchi.
Hissan Salum Iddi.

0 comments:
Post a Comment