Sunday, April 5, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Yanga na Etoile zote ziliwahi kumsajili kiungo mshambuliaji wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Okwi na kuzisababishia hasara kubwa.'

RASMI! Kila kitu kiko wazi kwamba Yanga SC itaikabili Etoile Du Sahel FC katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya timu hiyo ya Ligi Kuu ya Tunisia kuing'oa Benfica de Luanda ya Angola.

Baada ya Yanga SC kuwang'oa wachimba Almasi wa Zimbabwe, FC Platinum kwa jumla ya mabao 5-2 jana, leo Etoile du Sahel wameing'oa Benfica kwa jumla ya mabao 2-1 wakishinda 1-0 mjini Tunis, Tunisia miezi mwezi uliopita kabla ya leo kutoka sare ya 1-1 Angola.

Yanga SC wataanzia nyumbani Tanzania Aprili 17 kabla ya kurudiana na Etoile du Sahel mjini Tunis, Tunisia Mei Mosi mwaka huu.

Etoile, moja ya klabu kongwe na tajiri barani Afrika, iliwahi kumsajili Emmanuel Okwi kwa dola za Marekani 300,000 (Sh. milioni 480) misimu miwili iliyopita kabla kiungo huyo mshambuliaji kutoka Uganda hajatimkia Yanga SC mwaka mmoja baadaye.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video