MWANASOKA bora wa dunia na mshambuliajiwa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo leo ameweka rekodi ya aina yake ya kufunga 'hat-trick' jumlisha mawili ya nyongeza yaani magoli matano (5) peke yake katika ushindi wa mabao 9-1 kwenye mechi ya ligi kuu La Liga dhidi ya Granada.

Ronaldo alifunga mabao hayo katika dakika ya 31', 36', 38',54 na 89.
Mabao mengine manne yamefungwa na Gareth Bale dakika ya 25', Karim Benzema dakika ya 52' na 56'.

Naye Diego Mainz alijifunga goli goli katika dakika ya 83'.
Bao pekee la kufutia machozi kwa Granada lilifungwa dakika ya 74 kupitia kwa Martinez Ibanez.
Rekodi kali ya Ronaldo leo ni kufunga 'Hat-trick' ndani ya dakika 8' tu.

Katika mechi nyingine, Valencia imetoka suluhu na Villareal.
Getafe na Deportivo La Coruna wanachuana muda, wakati Barcelona watakuwa ugenini mnajira ya saa 4:00 kwa saa za Tanzania kuchuana na Celta Vigo.


0 comments:
Post a Comment