Sunday, April 5, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Mgambo Shooting inayonolewa na Bakari Shime, imepanda hadi nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu ya Bara ikifikisha pointi 27.'

MGAMBO Shooting Stars imefuata nyayo za Arsenal baada ya kuichapa mabao 4-0 Polisi Moro FC katika mechi ya Ligi Kuu ya Bara Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo jioni.

Kwa ushindi huo, Mgambo iliyomtimua aliyekuwa kocha mkuu Adolf Richard, imepanda kutoka nafasi ya tisa hadi ya sita ikifikisha pointi 27 baada ya mechi 20 wakati Polisi imeporomoka kwa nafasi moja hadi nafasi ya pili kutoka mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo.

Mabao ya Mgambo Shooting Stars yamefungwa na Fully Maganga dakika ya 31, Malimi Busungu dakika za 38 na 71 pamoja na Salim Aziz 'Gilla' dakika ya 76.

Polisi Moro FC wamemaliza tisa uwanjani baada ya refa Andrew Shamba kuwatoa kwa kadi nyekundu Anas Seleman dakika ya 51 na kipa Tony Kavishe dakika 65.

Ushindi huo pia ni faraja kwa jiji la Tanga ambalo jana lilihuzunishwa na kipigo cha bao 1-0 ambacho Coastal Union FC ilipewa na kikosi cha Mbwana Makata cha Tanzania Prisons FC.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video