Thursday, April 2, 2015


Na Bertha Lumala, Shinyanga
'Simba SC ilifungwa bao 1-0 na Stand United FC kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini hapa Februari 22, mwaka huu.'

Kopunovic anaska kisasi Kanda ya Ziwa! Ndivyo inavyonekana baada ya kocha mkuu wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic, kuwataka nyota wake waikazie Kagera Sugar FC katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini hapa Jumamosi.

Simba SC itasaka visasi viwili Jumamosi; kwa ni kuwafunga Kagera Sugar FC ambao waliichapa 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Novemba mwaka jana, shukrani kwa bao la Atupele Green.

Pili, kikosi cha Kopunovic kitasaka kisasi kwa kufungwa 1-0 dhidi ya Stand United FC kwenye Uwanja wa CCM Kamabarage Februari 22, mwaka huu, hivyo kinahitaji ushindi walau mmoja msimu huu Kanda ya Ziwa,

Kikosi chenye wachezaji 24 cha Simba SC kimeondoka jijini Dar es Salaam leo kuja mjini hapa kwa ajili ya mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Kagera Sugar huku kocha mkuu Kopunovic akiwataka nyota wake kutokujisahau tena na kuruhusu kufungwa usukumani.

Simba SC, mabingwa mara 18 wa Tanzania Bara, watakuwa na kibarua kigumu mbele ya kikosi cha kocha mkuu Mganda Jackson Mayanja cha Kgaera Sugar FC ambacho leo jioni kimeichapa Mtibwa Sugar FC mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kambarage na kuitumia salamu mbaya Simba SC.

Wakiwa safari kuja Shinyanga leo mchana, Msemaji wa Simba SC, Hajji Manara, amesema kuwa Goran amewataka wachezaji kuwa makini kuelekea mechi hiyo kwa vile ndiyo itakayoamua hatima yao katika mbio za ubingwa wa Bara msimu huu.

"Kocha mkuu (Goran) amesema mechi yetu inayofuata dhidi ya Kagera Sugar FC ni ngumu na ni muhimu kwetu kushinda ili tujiweke nafasi nzuri katika kuwania ubingwa na kumaliza nafasi nzuri katika msimamo wa ligi msimu huu," Manara amesema:

"Tunakwenda Shinyanga tukiwa na wachezaji 24, tunaiheshimu Kagera kwa sababu ni timu ngumu na ilitufunga mzunguko wa kwanza jijini Dar es Salaam. Tutapambana kusaka pointi zote tatu Jumamosi maana na sisi tuna kikosi kizuri kwa sasa."

Kagera Sugar FC ambao Jumamosi wataivaa Simba SC itakayomkosa beki fundi wa pembeni kulia, Hassan Kessy, ambaye amebaki Morogoro kutokana na kushindwa kuelewana na uongozi wa Simba SC, iliifunga timu hiyo ya Msimbazi bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Novemba mwaka jana na imepoteza mechi moja tu kwenye Uwanja wa CCM Kambarage tangu ihamishie maskani yake mjini hapa ikitokea Mwanza miezi miwili iliyopita.

Baada ya kucheza mechi 20, Simba iko nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 32, nane nyuma ya vinara Yanga na tano mbele ya Kagera Sugar walioko nafasi ya nne baada ya mechi 20.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video