Na George Mganga
Rwanda imeteuliwa kuwa mwenye wa fainali za kombe la
mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFGA Challenge Cup, Novemba
mwaka huu.
Katibu mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye amethibitisha uamuzi huo.
Rwanda inatazamia kutumia fainali hiyo kujiandaa kwa
michuano ya fainali za kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji
wanashiriki ligi ya nyumbani, maarufu kama CHAN.
Fainali hizo za CHAN, ndiyo ya pili kwa ukumbwa barani Afrika na
hushirikisha wachezaji chipukizi wanaocheza ligi mbali mbali nchini
mwao.


0 comments:
Post a Comment