Saturday, April 4, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Kabla ya kutua Ruvu Shooting Stars dirisha dogo Desemba mwaka jana, Tumbo alikuwa amefunga mabao saba katika Ligi Kuu ya Zanzibar.'

ANAJUA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mshambuliaji Yahya Tumbo wa Ruvu Shooting Stars kudhibitisha makali yake akiiongoza timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya ndugu zao JKT Ruvu Stars Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani leo jioni.

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Tumbo alifunga bao hilo dakika ya 54 akimalizia kwa shuti kali la mguu wa kulia krosi murua ya Michael Aidan na kupeleka kilio kwa kikosi cha kocha wa zamani wa Yanga SC, Fred Felix Minziro.

Hilo ni bao la tano kwa mshambuliaji huyo tangu ajiunge na maafande hao Desemba mwaka jana.

Magoli yake yamekuwa muhimu kwa kikosi cha Mkenya Tom Alex Olaba ambacho baada ya ushindi wa leo, kimepanda hadi nafasi ya tano kikifikisha pointi 26 na kuwaondoa mabingwa wa 1988 wa Tanzania Bara, Coastal Union FC ambao walikuwa katika nafasi hiyo kabla ya kulala 1-0 leo nyumbani dhidi ya Tanzania Prisons FC.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video