Saturday, April 4, 2015

MPIRA wa miguu raha mno! ukipenda huwezi kuacha kufuatilia!
Leo wakati wachezaji wa Simba na kocha mkuu Goran Kopunovic wakisubiri hatima ya mechi dhidi ya Kagera uwanja wa CCM Kambarage ambayo baadaye iliahirishwa kutokana na uwanja kujaa mvua kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, alitokea shabiki mmoja alivaa jezi za rangi ya Yanga, mwenye muzuka au kichaa cha kupenda soka.
Akiwa amedhamiria, shabiki huyo ambaye jina halikupatikana haraka alikaa nje ya uzio nyuma ya sehemu walipokaa wachezaji na kocha Kopunovic na kuanza kumwaga kiingereza cha kuungaunga mno huku akionekana kuyafahamu maneno machache.
"Kocha Kagera two, Simba no point!, Simba no point! Simba zero, aaaaaah! Mzungu me listen! Simba No Point alaaah! No playing oooh! Kagera two" Alisikika shabiki huyo.
Kopunovic na wachezaji wa Simba walibaki midomo wazi kwa kicheko.

Kila akimaliza kuzungumza maneno yake alipuliza vuvuzela na kucheka kwa furaha baada ya Kopunovic kuonekana amemuelewa.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video