Saturday, April 4, 2015



'Licha ya kufanya mabadiliko katika benchi la ufundi kwa kumtoa aliyekuwa kocha mkuu Mkenya James Nandwa na kumrejesha kundini kocha msaidizi Joseph Lazaro kutoka Africans Sports, Coastal imepoteza mechi ya pili mfululizo nyumbani Uwanja wa Mkwakwani.'

WAMEGOMA kuporomoka daraja! Ndivyo inavyoonekana kwa maafande wa Tanzania Prisons FC baada ya leo kupata pointi tatu ugenini walipoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Coastal Union FC Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo jioni.

Kwa ushindi huo ambao ni wa pili katika mechi tatu zilizopita tangu timu ianze kunolewa na Mbwana Makata, aliyerithi mikoba ya David Mwamaja aliyetimuliwa, Prisons FC imefikisha pointi 20 baada ya mechi 19 ikiendelea kubaki mkiani, lakini pointi moja nyuma ya Polisi Morogoro FC na Stand United FC zilizopo nafasi za 12 na 13.

Goli pekee la mechi hiyo limefungwa na Jeremia Juma dakika ya 45 na kuandika kipigo cha pili kwa kocha mkuu mwenhye maneno mengi Jamhuri Kihwelo 'Julio' tangu ajiunge na mabingwa hao wa 1988 wa Tanzania Bara miezi miwili iliyopita.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili Stand United FC wakiwa wenyeji wa Mtibwa Sugar FC Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga wakati Polisi Moro FC itakuwa mgeni wa wababe wa Simba SC, Mgambo Shooting Stars Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video