MLINZI wa kushoto wa Mtibwa Sugar, David Charles
Luhende amesema mechi tatu zilizobaki ambazo zote wanacheza nyumbani watafanya
vizuri na kushika nafasi za nne za juu katika msimamo.
Luhende alisema hayo jana baada ya timu yake
kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Prisons uwanja wa Sokoine Mbeya.
“Pointi moja sisi tunaona inatutosha kwasababu madhamuni yetu ilikuwa ni
kushinda , lakini mwamuzi mwenyewe alivyochezesha mechi kila mtu ameona, sasa
tumefikisha pointi 29, tunarudi nyumbani kucheza mechi zetu tatu zilizobaki na
mungu atasaidia kubaki kwenye ligi”, Amesema Luhende na kusisitiza: “Mwanzoni
tulikuwa tunapambana ili tuchukue ubingwa, ligi ilisimama na tukaa nyumbani kwa
muda mrefu na tuliporudi tena kambini Mungu hakutupa bahati, kila tulipokuwa
tunacheza mchezo tulikuwa tunapoteza kwa bahati mbaya, Mungu katujalia leo
tumepata pointi moja na mechi zilizobaki tutashinda, tuna uhakika wa kubaki ligi kuu na kuchukua
nafasi nne za juu”.


0 comments:
Post a Comment