Nyoso (aliyeruka juu) aliwadhabiti vizuri washambuliaji wa Simba
MOJA ya kikwazo cha Simba kufungwa 2-0 dhidi ya
Mbeya City katika uwanja wa Sokoine mwishoni mwa juma lililopita ni mlinzi wake
wa zamani ambaye sasa anakipiga kwa Wagonga nyundo wa Mbeya, Juma Said Nyoso.
Nyoso amesema hana chuki na Simba bali anafanya
kazi yake ipasavyo kwasababu inampatia ‘ugali’
“Sijali ni timu gani nacheza nayo, napenda kuwa
katika kiwango changu, nimefurahia kuisaidia timu yangu kupata ushindi, lengo
ni kushika nafasi za juu, tunaweza kufanya hivyo”, Amesema Nyoso na kusisitiza:
“Simba tuliwadhibiti sehemu zote, nilikusudia kutowapa nafasi, hata angekuwepo
Okwi (Emmanuel) asingefua dafu, tulijipanga vizuri”.


0 comments:
Post a Comment