MBWANA Makata, kocha mwenye uzoefu wa kufundisha
timu za majeshi safari hii amepewa jukumu la kuibakisha Tanzania Prisons ligi
kuu Tanzania bara msimu ujao.
Makata, kocha wa zamani wa JKT Ruvu na JKT Oljoro jana
ameiongoza Prisons kupata sare nyumbani ya goli 1-1 dhidi ya Wakata miwa wa
Mtibwa Sugar katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa uwanja wa CCM Kumbukumbu ya
Sokoine, Mbeya.
Baada ya sare hiyo, Makata amesema: “Mechi ilikuwa
ni muhimu kwetu kuweza kupata matokeo ya ushindi, lakini mechi ilikuwa ngumu na
tumeweza kutapa sare ya goli 1-1. Kikubwa niwapongeze vijana wangu kwasababu
ratiba kwetu ilibana wiki hii, tulicheza jumatano, tukawa safarini na kucheza
tena leo (jana), muda wa maandalizi haukuwepo. Cha msingi niwaombe wakazi wa
Mbeya, mashabiki wa Prisons waisapoti timu yao, tupambane mpaka dakika za
mwisho tuone nini kitatokea”


0 comments:
Post a Comment