NAHODHA
wa Simba, Hassan Suleiman Isihaka anaumwa maralia na Typhoid na amesisima
kufanya mazoezi madogo madogo aliyoanza kwa ajili ya kuimarisha mguu wake.
Isihaka akiwa na daktari wa Simba, Yassin Gembe siku aliyoumia
Beki huyo mstaarabu aliyeumia
aprili 18 mwaka huu Simba ikifa 2-0 dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa
Sokoine na kutolewa nje dakika ya 23’, ameiambia MPENJA BLOG kuwa ameshapima Hospitali na sasa yupo kwenye dozi.
“Ninasumbuliwa
na maralia na typhoid, ilinianza jumamosi baada ya mechi dhidi ya Ndanda fc,
nimeenda Hospitali na kupatiwa dawa”. Isihaka ameuambia mtandaon huu na
kuongeza:“Mguu unatengamaa fresh, lakini tatizo ni malaria, nilishaanza mazoezi
madogo madogo, lakini sahizi naumwa”
Mlinzi
huyo kipenzi cha kocha wa Simba, Goran Kopunovic amewatakia kila la kheri
wachezaji wenzake kuelekea mechi ya mwishoni mwa juma hili.
“Mimi
niwatakiwa kheri wachezaji wenzangu kwenye mechi ya jumapili dhidi ya Azam fc,
naamini watacheza vizuri na kushinda ‘inshaallah’”
Isihaka
toka aumie amekosa mechi mbili dhidi ya Mgambo JKT waliyoshinda 4-0 na ile ya
Ndanda fc ambayo Simba waliibuka kidedea kwa magoli 3-0.
Kutokana
na kukosekana kwa Isihaka, Kopunovic anawatumia walinzi wawili wa kati kutoka
Uganda, Juuko Mursheed na Joseph Owino.
0 comments:
Post a Comment