Chidiebele mwenye jezi namba 9 kwenye bukuta
MNIGERIA
anayekipiga ‘chama la wana’ Stand United, Abasalim Chidiebele amekiri kukumbana
na changamoto kubwa kutoka kwa mabeki wa timu za ligi kuu soka Tanzania bara.
Chidiebele
ambaye ameifungia Stand United magoli 9 mpaka sasa ameiambia MPENJA BLOG kuwa walinzi wa timu za ligi
kuu wanajua kuwa yeye ndiye mshambuliaji tishio katika timu yake, hivyo
wanamkaba ipasavyo kuhakikisha hawadhuru.
“Walinzi
wa timu pinzani wanajua kuwa Chidiebele (Abasalim) ni mtu hatari Stand United,
wananikaba na kuninyima nafasi ya kufunga, kila mechi mabeki wananiangalia sana”
Amesema Chidiebele na kusisitiza kuwa “Mimi ni mshambuliaji, natafuta janja
zangu na kuwaadhibu, najua huu ni mchezo wa kulipwa. Sahizi nafanya juhudi ya
kuisaidia timu yangu kubaki ligi kuu, haya ndiyo malengo yangu makubwa”.
Stand
United ipo kwasasa ipo nafasi ya 11 ikijikusanyia pointi 28 katika mechi 24
walizocheza.
Timu
hiyo ya wapigadebe wa Shinyanga mjini imebakiza mechi dhidi ya Coastal Union
uwanja wa Mkwakwani tangu itayochezwa jumapili hii na mechi ya mwisho ni mei 9
mwaka huu watapochuana na Ruvu Shooting uwanja wa nyumbani wa CCM Kambarage
Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment