YANGA SC
wameondoka usiku wa jana kwenda nchini Tunisia kupitia Dubai kuwafuata
wapinzani wao Etoile du Sahel.
Etoile
na Yanga zitachuana keshokutwa katika mechi ya marudiano ya hatua ya 16 bora ya
kombe la shirikisho baada ya kutoka sare
ya 1-1 mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es salaam takribani wiki
mbili zilizopita.
Yanga wanahitaji
ushindi au sare ya kuanzia magoli 2-2 ili kusonga mbele moja kwa moja.
MPENJA BLOG ilikuwepo uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakati Yanga wanakwea ‘pipa’
na ulipata nafasi ya kuzungumza na kocha Hans van der Pluijm.
“Hatuna
cha kupoteza kwenye mchezo huo, tulitoka sare ya kufungana goli 1-1 tukiwa
nyumbani hivyo tunahitaji kupata ushindi au sare ya magoli kuanzia mawili ili
tuweze kusonga mbele. Tumejipanga vizuri kwa hili na wachezaji wote tunaokwenda
nao wanatambua umuhimu wa mchezo huo”, alisema Pluijm na kusisitiza: “Etoile ni
timu nzuri na ina uzoefu mkubwa kwenye michuano ya Afrika na kila mtu aliona
aina ya soka walilocheza hapa, tunawaheshimu na tumejipanga ili kukabiliana nao
na kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
“Ni lazima tucheze soka la kushambulia na
kupata magoli ya mapema lakini wakati huohuo tunatakiwa kuwa makini sana
kuhakikisha haturuhusu kufungwa goli, nimezungumza na wachezaji na kila mtu
anajua majukumu yake. Najua kwenye soka lolote linaweza kutokea na tukasonga
mbele kwa hatua inayofuata”.
Ukiyasoma
maneno hayo ya Pluijm kuna mambo matatu anayochukulia uzito wa hali ya juu;

Mosi,
kujiamini ndio silaha ya mafanikio; Pluijm anaposema hawana cha kupoteza zaidi
ya kutafuta ushindi ugenini tena wa magoli mengi ni ishara ya yeye mwenye
kujiamini na kwa maana hiyo hata wachezaji wake wamejiamini.
Wataalamu
wa mpira wanasema wachezaji wanacheza kuakisi falsafa ya mwalimu, kama mwalimu
atahofia mechi na kuonesha hofu yake kwa wachezaji basi na wao watahofia. Kocha
akijiamini hata wachezaji watajiamini pia. Pluijm ameonesha kujiamini zaidi na
hana shaka na mechi hiyo.
Pili;
Pluijm anafahamu ubora wa wapinzani wao, yeye ni kocha, aliwaona mechi ya
kwanza na kubaini wana uzoefu mkubwa na muunganiko wa timu, kwa maana hiyo
ataingia uwanjani kwa tahadhari kubwa akijua anacheza na timu bora.
Tatu;
anajua faida ya kutofungwa mapema, kushambulia na kikubwa zaidi ni kucheza kwa
nidhamu kwa lengo la kujilinda. Makocha wengi wanakosea katika mipango ya
mechi, anawahamasisha wachezaji kushambulia kwasababu anahitaji matokeo, lakini
anashindwa kuwakumbusha kwa haraka wachezaji wake kuhusu nidhamu ya ulinzi.
Pluijm anasema watashambulia na kujilinda kwa nidhamu ya hali ya juu, hilo ni
jambo muhimu.
Lakini
mbali na hayo, Mtandao huu unaheshimu uwezo wa mabingwa wa Tanzania, Dar Young Africans, wanaweza kushinda, kutoa
sare au kufungwa kutokana na kikosi chao kuwa na wachezaji wenye uwezo binafsi
na kimekaa kwa pamoja angalau kwa muda mrefu.
Amissi
Tambwe, Mrisho Ngassa, Simon Msuva ni wachezaji wanaoweza kuamua matokeo kwa
kutegememea ubora wa Haruna Niyonzima na Salum Telela dimba la kati.
Etoile
du Sahel ni timu bora barani Afrika, ina wachezaji wazuri kwa kuangalia kipaji
cha mchezaji mmoja mmoja bila kusahau muunganiko wa timu ‘Team Chemistry’.
Wanaweza
kujilinda, kudhibiti kiungo cha mpinzani, kupiga pasi za kupenyeza, kutengeneza
mashambulizi na kumalizia kazi yao kwa ustadi mkubwa.

Kutokana
na ubora wao na uzoefu wao katika soka la kimataifa kunafanya watu wengi
wawadharau Yanga na kuona wanaenda kufa nyingi Tunisia. Kimajina, hakuna
ushindani baina ya timu hizi, Etoile ni timu kubwa yenye mafanikio kuliko Yanga
kwa ngazi ya kimataifa, lakini lazima ukumbuke kuwa huu ni mpira, chochote
kinaweza kutokea.
Inatokea
mara nyingi timu bora inapoteza, mpira wa miguu ni mchezo wa makosa, unaweza
kuongoza kwa kila kitu, umiliki wa mpira, mashuti yaliyolenga lango, mashuti
ambayo hayakulenga lango, kona nyingi, lakini ukafungwa goli moja tena la
kukuotea tu na mwisho ukapoteza mechi.
Yanga
wanaweza kushinda wakijiamini, lazima watashambuliwa sana, lakini ni kawaida
katika soka hususani unapokuwa ugenini, cha msingi ni kuwa na nidhamu ya ulinzi
na kujitahidi kuua viungo wa Etoile wasisambaze mipira kwa viungo wao
washambuliaji na washambuliaji wa kati.
Timu za
uarabuni ni maarufu sana kwa mipango ya nje na ndani ya uwanja, wanajua namna
ya kumtoa mpinzani mchezoni, wanajua namna ya kucheza na waamuzi.
Unaweza
kutua uwanja wa Ndege ukakalishwa saa nne bila kumuona mwenyeji wako halafu
baadaye ukaletewa basi bovu, ukanyimwa uwanja mzuri wa mazoezi, lengo ni kukufanya uathirike
kisaikolojia.
Wanajua
wazi kuwa mchezaji anaweza kuwa na ufundi, mbinu, utimamu wa mwili, lakini
akiwa hovyo kisaikolojia anafanya vibaya.
‘Uchawi’
pekee wa Yanga kushinda ni kutegemea kufanyiwa‘fitina’, lakini ‘wasipaniki’
wajue uarabuni ni mahala pa fitina. Unajua ukijitayarisha kwa jambo baya
unalokwenda kufanyiwa na mpinzani wako na kujiandaa kupamabana nalo kama
changamoto ya kawaida, unaifanya akili iwe sawasawa. Cha msingi wajiandae kisaikolojia
kupambana nao, wawapotezee kwa mambo yao mabaya, wachukulie ni changamoto tu.
Viongozi, makocha, wachezaji waelekeze nguvu
kwenye mchezo, wasifirikie fitina, wasikae kiunyonge hotelini na wachezaji,
wasiwahusishe wachezaji kwa mambo wanayoyaona kama viongozi, wakianza kufirikia
kuwa wanafanyiwa fitina na kuwaeleza wachezaji kuwa wanaonewa, watakuwa
wameingia kwenye mtego wa Etoile na watashindwa kufanya vizuri.
Hata
wakiingia uwanjani jumamosi wakiona kama mwamuzi hayuko upande wao, wacheze
soka la kuwatoa wapinzani kwenye eneo lao, wasiwape upenyo mapema wa kuingia
kwenye eneo la hatari, kwasababu wakifanya hivyo wachezaji wa Etoile wanaweza
kujiangusha na kupewa penalti au faulo za mapema.
Ikitokea
hivyo maana yake Yanga watakuwa na uwezekano wa kufungwa mapema na kuondoka
mchezoni.
MPENJA BLOG inawatakiwa kila la kheri Yanga!
Maoni: 0712461976
Maoni: 0712461976
0 comments:
Post a Comment