Maguri (kushoto) akiwa na Awadhi Juma
MSHAMBULIAJI
mwenye nguvu na kasi wa Simba, Elius Maguri amesema kamwe hawezi kukataa tamaa
kutokana na kitendo cha kocha mkuu wa klabu hiyo, Mserbia Goran Kopunovic
kumuweka benchi watoto wa mjini wanaita 'kochoma mahindi' katika mechi za ligi kuu Tanzania bara zinazoendelea kurindima wat
Simba
imebakiza mechi mbili tu za ligi kuu dhidi ya Azam fc jumapili hii na JKT Ruvu
mei 9 mwaka huu na sahizi ipo nafasi ya tatu ikijikusanyia pointi 41 baada ya
kucheza mechi 24, pointi nne nyuma ya Azam fc waliocheza mechi 23.
Hata
hivyo Maguri aliyekuwa kipenzi cha kocha aliyeondoka Simba, Patrick Ackson
Phiri ameiambia MPENJA BLOG kuwa hana
uhakika wa kucheza mechi hizo na yeye mwenyewe amekiri kutozifikiria
“Kwenye
mpira wa miguu kuna wakati unapata nafasi na wakati mwingine hupati, kila
mwalimu ana falsafa yake, lakini mimi siwezi kukata tamaa, napambana, nafanya
mazoezi kwa bidii”. Amesema Maguri na kuongeza: “Kama Mungu atajaalia tukawa
pamoja msimu ujao, watu watarajie mambo mazuri. Hutajawi kukaa na mwalimu Kopunovic
(Goran) kuzungumza kuhusu suala langu, lakini ni mwalimu mzuri, anajua
kufundisha, mhamasishaji, pamoja na kufundisha timu vizuri, kikubwa kwake
anajua namna ya kuhamasisha”.
Mshambuliaji
huyo wa zamani wa Tanzania Prisons na Ruvu Shooting aliyesajiliwa na Simba majira
ya kiangazi mwaka jana amesema kwasababu mechi zimebaki mbili hataki
kuzungumzia kwanini hatumiki, lakini msimu mpya utakapoanza itabidi ajue
mstakabali wa kupata nafasi ya kucheza.
“Najisikia
vibaya sana tunapopoteza mechi halafu mimi nataka nicheze kuisaidia timu yangu,
inauma sana ukizingatia nilisajiliwa ili niisaidie timu yangu, lakini wanaingia
wachezaji 11 na wengine wanabaki wa akiba, mwalimu yeye ndiye anaona nani
acheze na nani abaki”.
Maguri mpaka sasa ameifungia Simba magoli matatu (3) msimu huu.
0 comments:
Post a Comment