STRAIKA mkali wa magoli ya vichwa wa Mbeya City fc
ambaye msimu huu hana nafasi katika
kikosi cha kwanza , Mwegane Yeya alisema haya baada ya timu yake kufungwa
magoli 3-1 jana dhidi ya Yanga uwanja wa Taifa Dar es salaam;
“Kwakweli
ligi ya safari hii imekuwa ngumu sana na isitoshe tulikuwa ugenini na Yanga
walikuwa nyumbani, tukubali kuwa tulizidiwa. Mpira unapofanya makosa sehemu Fulani
mwenzako ndio anatumia”
“Wenzetu walipata nafasi na kuweza kuzitumia, sisi
tulipata hatukutumia, kwahiyo tunakubali matokeo, lakini tunaomba
mashabiki tufike mahali tujipange kwa
mechi zingine zinazokuja ili tuweze kushinda”
“Tuna upungufu wa muda, nadhani mwalimu atatumia
vizuri muda ili kujiandaa kwa mechi ijayo ya Simba, wala sio tatizo na
tunaamini tutashinda mechi hiyo”.


0 comments:
Post a Comment