NADIR HAROUB ALI ‘Cannavaro’ , nahodha wa Young Africans alifunga goli moja katika ushindi wa 3-1 waliopata Yanga dhidi ya Mbeya City jana uwanja wa Taifa.
Magoli mengine yalifungwa na Kpah Sherman na Salum
Telela wakati la Mbeya City lilifungwa na Themi Felix.
Cannavaro ‘Baba mwenye nyumba’ safu ya ulinzi ama
kamanda wa ngome ya ulinzi ya Yanga baada ya mechi hiyo ametamka kauli mbili
kubwa;
Moja ni kuhusu upinzani walioonesha Mbeya City fc
ambapo amesema:
“Mimi nasema kwamba watu wa mbele waongeze
umakini, ila tu Mbeya City ni timu nzuri, wamecheza vizuri sana, ila sisi ni
wazuri zaidi yao, nafasi imepatikana na tumetumia”.
Kauli ya pili ni kuhusu mechi ya kombe la
Shirikisho dhidi ya Etoile du Sahel itayopigwa wikiendi ya wiki hii, Cannavaro
amesema: “Bado tuna mchezo mgumu wa kimataifa (kombe la Shirikisho dhidi ya Etoile
du Sahel ya Tunia) na tunajiandaa kwa ajili ya mchezo huo”
Cannavaro ni miongoni mwa mabeki wa kutumainiwa wa
Yanga na amekuwa kiongozi mzuri wa kuhamasisha timu kila inapocheza, iwe mechi
za ligi kuu au za kimataifa.
Pia ni mchezaji muhimu timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa
Stars’.

0 comments:
Post a Comment