FRENCH daily L’Equipe amefichua stori ya kusikitisha mwisho mwa wiki hii kumuhusu gwiji wa Brazil aliyeshinda kombe la dunia.
Paulo Cesar, anayejulikana kwa jina la Caju ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi maarufu cha Brazil kilichoshiriki kombe la dunia mwaka 1970.
Kwa ujumla, Caju aliichezea nchi yake mechi 57 akifunga magoli 10 katika miaka 10 ndani ya kikosi cha Brazil.
Katika kiwango cha klabu, Paulo Cesar alizichezea klabu za Botafogo, Flamengo, Fluminense, Gremio, Vasco da Gama, Corinthians, na alicheza kwa msimu mmoja katika klabu ya Ufaransa, Marseille msimu wa 1974 – 1975.
Baada ya kumaliza maisha ya soka, mwanasoka huyo wa zamani mwenye miaka 65 amekuwa na maisha magumu na ukweli umethibitika siku za karibuni kuwa ameuza medali yake ya dhahabu iliyoshinda mwaka 1970 katika fainali za kombe la dunia ili anunue dawa za kulevya aina ya cocaine.
L’Equipe amemnukuu Paulo Cesar akifichua habari hizi zilizogonga vichwa vya watu wengi na hapa tumetoa tafsiri isiyokuwa rasmi:
"Siwezi kuzuia hisia zangu.Kamwe sikufanya mazungumzo wakati nauza medali zangu za dhahabu. Hii ni hasara kubwa".
"Sijawahi kumwambia mtu yeyote (kwamba niliuza medali zangu za kombe la dunia), lakini sasa nataka watu wajue. Cacaine zilikuwa muhimu kwangu kuliko medali".
UJUME WA KIINGEREZA HUU HAPA CHINI
"I had no emotional control. I never had to negotiate and sell precious medals. This is a huge loss!
I’ve never told anyone [that I sold my World Cup medal], but now I’m going to let people know. Cocaine was most important for me, the medal was less.


0 comments:
Post a Comment