GWIJI wa Santiago Bernabeu, Zinedine Zidane ambaye ndiye kocha mkuu wa Real Madrid B maarufu kwa jina la Castila B ingawa pia ni kocha msaidizi wa timu kubwa amesisitiza kuwa timu yake ina nia ya dhati kunasa saini ya winga wa Liverpool na England, Raheem Sterling.
Liverpool wapo katika mazungumzo na Sterling ambaye juzi juiz tu alikataa ofa ya kulipwa paundi laki moja (100,000) kwa wiki katika mkataba mpya anaoombwa kusaini.
Mpaka sasa bado hawajafikia makubaliano ya mkataba mpya na Zinade na timu yake wapo makini kufuatilia mpango mzima.

Zidane (kushoto) akiwa katika benchi na kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti
Sterling msimu huu amefunga magoli 6 na ameonesha kipaji cha hali ya juu licha ya umri wake kuwa mdogo.
Zidane ametumia mfano wa usajili wa karibuni waliomnasa Gareth Bale, Raphael Varane kuwa unaonsha jinsi gani wamekusudia kunasa wachezaji nyota vijana wa dunia hii na ameweka wazi kwamba kwasasa wanamtaka Sterling.
"Tunajua Sterling ni mchezaji wa aina gani, kiukweli tunafuatilia nyendo zake na Liverpool' Amesema Zidane.


0 comments:
Post a Comment