Thursday, April 30, 2015


Rais wa Simba, Evans Aveva

Na George Mganga, Dar es salaam
Nazidi kutoa pongezi zangu za dhati kwa wasomaji wa makala zangu kadri siku zinavyokwenda na pongezi ambazo zimekuwa zikiniijia kwa kile ninachokiandika hapa.
Tupo hapa kuandika yale yote yanahosiana na soka letu ili kuhakikisha tusonga mbele na sio kurudi nyuma na siku zote mwanadamu huwa na attention ya kusonga mbele.
Kikubwa ninachoanza nacho leo ni mustakabali wa klabu ya Simba ulivyokuwa kwa msimu huu wa 2014/2015 kuwa moja ya msimu wenye au uliokuwa na changamoto joto kabisa kuwahi kutokea katika klabu hii.
Wakati Ismail Aden Rage akiwepo madarakani akiwa kama Mwenyekiti wa klabu ya Simba ukiachilia sasa nafasi hiyo imegeuzwa na wadhifa huo kupewa hadhi ya Uraisi alikuwa amelenga zaidi kuimarisha kikosi B.
Rage alipenda kuona Simba inabajeti vizuri mikakati yake ikiwemo na matumizi mazuri ya fedha kwaajili ya timu na shughuli zingine ndani ya timu hiyo.
Alilenga zaidi kuimarisha kikosi B ili kupunguza zaidi matumizi mabaya ya fedha kwaajili ya usajili wa wachezaji kutoka sehemu zingine na badala yake aliwainua zaidi vijana hao na kuwaleta Simba B.
Tuaona uongozi huu ambao umekuja kimfumo tofauti zaidi ambapo wamekuwa na nguvu ya kutumia pesa zaidi kuliko kuendeleza soka la kikosi cha pili kwa kusajili wachezaji ambao hata nafasi ya kucheza wanakuwa hawapati.
Aidha pia klabu inakuwa inatumia pesa nyingi sana hata kufikia wakati sasa hali ya uchumi kuyumba klabuni hapo na kuanza kusababisha madeni na hata hasara kwa mikakati hiyo.
Hili linarudisha nyuma sana maendeleo ya timu na ukiangalia hii timu ni kongwe huku mambo inayofanya hayaendani kabisa na hadhi ya timu.
Udhaifu wa kilabu kutafuta wadhamini pia nalo hili ni changamoto kubwa, Simba hii inategemea zaidi TBL kama mdhamini wake mkubwa na hawana hata mbinu zingine za kutafuta chanzo vya fedha jambo ambalo hapa juzi tu limesababisha kusikika kwa kauli tata ya kuyumba kwa uchumi.
Kama timu inatakiwa kujijenga basi haina budi kuwa na vyanzo vya fedha na klabu ni brand au nembo ambayo inaweza ikaanzisha mradi kupitia bidhaa zake.
Tanzania hii ina mashabiki wengi mno wa Simba na sidhani kama hawawezi kununua bidhaa za timu hiyo kutokana na ukubwa wa jina lake.
Tunawaona raia wa wamepata nafasi ya kuitumia fursa ya kuuza jezi za timu na vifaa mbalimbali vya timu bila timu yenyewe kuwa na mdhamini maalum wa kusimamia mauzo ya jezi na bidhaa mbalimbali za timu.
Kama bidhaa za timu zitasimamiwa ni motisha tosha ya kipato kuongezeka katika klabu na kuua madhaifu yote ambayo yamekuwa yakisikika na hata wachezaji sasa kutimiziwa mahitaji yao.
Suala la betting au kamali nalo pia linahusika tena kwa asilimia kubwa tu, uwezekano wa viongozi tena wao kwa wao kucheza kamali ilimradi tu wapige hela lipo kabisa bila magumashi yotote huku mashabiki wenye uchungu wanaolipa ada yao ya uanachama wanaumia kila siku.
Kitu kingine kikubwa kinachoisibu Simba ni ubabe kwa viongozi jambo ambalo linaleta au kusababisha viongozi wao kwa wao kutofautiana na kuleta matokeo sio mazuri katika timu.
Kiongozi na kiongozi wote kwa ujumla hawana budi kushikamana na kuungana vizuri kwaajili ya kuweka sera sawa ili kuunda timu ifike mbali na kupanga mikakati chanya kwaajili ya faida timu.
Kitendo cha kiongozi mmoja kuamua kufanya usajili bila hata ya kuwajumuisha viongozi wengine kisa tu ana mahaba au imani na mchezaji ambaye anamtambua haileti tija.
Licha ya hilo pia suala la matabaka katika timu ndiyo linaiua Simba hii kabisa na hili lilitokea mapema baada ya uchaguzi kukamilika na hatimaye kuanza kazi huku wanachama wengine wakiwa wamejitenga.
Utofauti wa viongozi na wanachama unathiri timu nje na hata ndani ya uwanja, sasa tunaona asilimia ndogo ya mapato ikipatikana uwanjani kutokana na uongozi kugawa hawa wanachama.
Nadhani tunakumbuka kabisa Aveva aliwafuta baadhi ya watu wanachama kwa kosa la kwenda mahakamani jambo ambalo limesababisha hata wingi wa mashabiki kwenda uwanjani kupungua ukiliachilia mechi ambayo huwa wanacheza na Yanga pekee.
Timu ikiwa imeunganika vizuri, katika pyramid nzuri kuanzia viongozi, wadhamini, wanachama, mashabiki pamoja na wachezaji inaleta ari nzuri sana katika timu na hata wachezaji huwa na morali nzuri katika uwepo wao.
Matabaka kwa wachezaji pia imekuwa ni suala sugu katika klabu ya Simba, tunaona kabisa klabu haitoi mahitaji sawa kwa wachezaji wote.
Mchezaji fulani anachukuliwa ana thamani kubwa tofauti na mwingine jambo ambalo halifai kabisa, unapoweka matabaka na kumuona mchezaji fulani ndiyo nyoya na hata kuwatenga wengine lazima timu iboronge.
Ili timu ifanye vizuri hakuna budi ya kuwajumuisha vizuri wachezaji wote na kuwapata mahitaji yao muhimu kwa pamoja sababu wote hawatokuwa na roho ya kwanini huyu au kwanini yule anafanywa hivi.
Klabu pia haina budi kuwa na malengo ya muda mrefu, malengo ambayo yapo kufanya timu ifike mbali na hili mfano mzuri ni pindi Simba inapojiandaa na mechi ya Yanga kumekuwa na matumizi mabaya ya fedha na maandalizi yamekuwa yakifanywa kwa asilimia 100 ili kufunga Yanga tofauti na vilabu vingine.
Kikubwa sasa msimu wa ligi umeisha ninachokiomba ni umoja ndani ya timu na mshikamano virudi na kama haya yatazidi kutendeka basi tutazidi kuona Simba ikipotea kabisa.
Ni halali yako kushea nami mawazo yako kwa kile nilichokiandika hapa kwa kunipata na hii namba.
0688665508

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video