Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Mwamaja aliwahi kuinoa Simba 1999, mwaka ambao Mtibwa Sugar FC ilitwaa kwa mara ya kwanza taji la Tanzania Bara.'
KOCHA aliyefukuzwa kazi katika timu ya Tanzania Prisons, David Mwamwaja, amesema yupo katika mikakati ya kutafuta timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwa ajili ya kuifundisha msimu ujao.
Mwamwaja aliyewahi kuinoa Simba 1999, ameuambia mtandao huu leo kuwa ukocha ndiyo fani yake aliyoisomea, hivyo hana budi kuifanyia kazi kwa kutafuta timu nyingine ya kufundisha baada ya kutimuliwa Prisons licha ya kuinusuru timu hiyo isishuke msimu uliopita baada ya kuichukua kutoka kwa Mbwana Makatta aliyerejeshwa.
“Siwezi kuacha kazi yangu niliyoisomea, kwa kuwa nimefukuzwa Prisons, naamini nina uwezo mkubwa wa kuipa timu yoyote mafanikio endapo nitapewa ushirikiano na kila kitu cha muhimu ambacho kinastaili kuwepo katika timu hivyo naweka milango wazi kwa timu yoyote ambayo itanihitaji, nipo tayari,”amesema Mwamwaja.
Mwamwaja akiwa Prisons ,aliambulia pointi sita katika mechi 19 alizoiongoza timu hiyo msimu huu kabla ya uongozi kuamua kumtupia virago na nafasi yake kupewa Makatta.
0 comments:
Post a Comment